Habari zenu wapendwa!!!!
As proudly mchaga, leo nawaletea historia ya wachaga... Chanzo cha habari izi ni makumbusho ya taifa na kumbukumbu za kale .....
ASILI YA KABILA LA WACHAGA
Kabila la Wachaga linafahamika kwa wengi
kuwa linapatikana mkoani Kilimanjaro. Kwa
asili, Wachaga ni mchanganyiko wa Wamasai,
Wasambaa, Wataita, Wakamba na Wakahe.
Wachaga walianza kuhamia kwenye miteremko
ya Mlima Kilimanjaro kwenye karne ya 17.
Walipofika wakiwa katika vikundi vidogovidogo
waliwakuta wakazi, wenyeji kwenye Misitu ya
Mlima Kilimanjaro walioitwa Wakonyingo.
Wenyeji hawa ambao huitwa Mbilikimo
hawakupenda kuchanganyika na wahamiaji
wageni, hivyo wakahama na kuanzisha makao
yao ya kudumu kwenye misitu minene iliyopo
nchini Kongo.
Watu wengi wanafikiria kwamba Wachaga
wanatokana na asili moja. Ukweli ni kwamba
wamegawanyika katika himaya 15,
wanatofautiana kwa lafudhi, lugha, rangi na
mwonekano wa miili yao. Wachaga wapo katika
makundi makuu matatu ya Hai, Vunjo na
Rombo.
Wale wanaopatikana eneo la Hai ni Wasiha,
Wamasama, Wamachame,Wangíuni, Wakibosho,
Wauru na Wamoshi. Kwa wale wanaopatikana
eneo la Vunjo ni Wakirua, Wakilema,
Wamarangu, Wamamba na Wamwika.
Kutoka eneo la Rombo ni Wamkuu, Wamashati
na Wasseri.
Hadi sasa haijulikani vizuri asili ya jina
Wachaga, ila wanahistoria wanaeleza kwamba
jina hilo linatokana na neno la Kiswahili
linaloitwa 'Kichaka'.
Inaelezwa kwamba misafara ya
wafanyabiashara iliyokuwa ikiongozwa na
Waswahili pamoja na Waarabu, walipokuwa
wakipita maeneo ya Vunjo waliwaona wenyeji
wa huko wakiwa wamejenga vibanda vya
kulinda mazao yao yasiliwe na wanyama
waharibifu.
Wakawaita wenyeji hawa kwamba wanaishi
vichakani na kuanzia hapo wageni
wafanyabiashara na Wamisionari walipokuwa
wanakuja Kilimanjaro walielekezwa na
waongozaji misafara yao kwamba wanakwenda
kwenye nchi ya “Uchakani”, wakimaanisha
kwamba kwa watu wanaoishi vichakani.
Hatimaye wageni wakashindwa kulitamka vizuri
neno hili na kuliita ìUchagani,
Jina hili likawekwa kwenye ramani na kuitwa
nchi ya “Wachaga”. Hivyo ndivyo wenyeji
waliokuwa wakiishi kwenye Miteremko ya Mlima
Kilimanjaro walivyopewa jina lao. Wachaga.
Maendeleo ya Wachaga
Maendeleo yao hapo awali yalitokana na zao la
kahawa. Walifanikiwa kuanzisha vyama vya
ushirika na hatimaye mwaka 1932 walianzisha
Halmashauri ya Wachaga (Chaga Council)
ambayo kwa sasa inatumiwa na Halmashauri
ya Wilaya ya Moshi. Halmashauri hii iliongozwa
na Mangi Mkuu Mshumbue Thomas Marealle II.
Mwaka 1946, utawala wa Waingereza
uliboresha Baraza la Halmashauri ya Wachaga.
Himaya ndogo za Wachaga zipatazo 17
(himaya mbili za Wakahe na Waarusha chini
zilijumuishwa kwenye Tarafa ya Vunjo) na
kuundwa kwa Tarafa tatu za Hai, Vunjo na
Rombo.
Halmashauri ya Wachaga ilijenga miundombinu
na huduma za jamii ikiwamo kuwasomesha
watoto wao kwenye shule na vyuo mbalimbali
kama Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.
Halmashauri ya Uchaga ilikuwa na bendera
yake ambayo ipo hadi leo kwenye Halmashauri
ya Wilaya ya Moshi, yenye nembo tano kuu:
1. Mlima Kilimanjaro uliochorwa katikati ya
bendera ukionyesha mandhari nzuri ya kilele
cha Kibo. Kilele cha Kibo kinatoa maji safi na ni
kielelezo cha umoja wao.
2. Chini ya kilele cha Kibo, upande wa kushoto
wa bendera kuna mgomba wenye ndizi. Hiki ni
chakula kikuu cha Wachaga.
3. Upande wa kulia wa bendera ni tawi la mbuni
ukiwa na matunda yake. Kahawa ni zao
lililowaletea maendeleo.
4. Bendera imezungukwa na matawi ya 'sale'
lenye matawi mawili (draceana plant). Matawi
haya yamefanya mduara kuzunguka kilele cha
Kibo, mgomba wa ndizi na tawi la zao la
kahawa. Masale ni mmea unaoheshimiwa sana
na Wachaga wote.
Ni alama ya amani. Masale hutumika katika
sherehe na shughuli zote za kimila
zinazofanywa na Wachaga. Majani yake ni
kijani kibichi yanayoonyesha jinsi Kilimanjaro
ilivyo na rutuba nzuri inayostawisha mazao ya
kila aina.
5. Juu kidogo ya kilele cha Kibo yupo chui
ambaye amejipumzisha. Chui ni alama kuu ya
mamlaka ya Wachaga.
Hapo awali kwenye miteremko ya Mlima
Kilimanjaro walikuwepo chui wengi wa rangi
nyeusi lakini kutokana na ongezeko la watu
pamoja na uharibifu wa mazingira chui hawa
wametoweka.
Sikukuu ya Wachaga
Sikukuu ya Wachaga wote ilikuwa
ikiadhimishwa Novemba 10 kila mwaka kama
kumbukumbu ya siku ambayo Wachaga wote
walipokusanyika na kumchagua Mangi Mkuu
baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya
Uchaga.
Maadhimisho ya kwanza ya mwaka 1952
yalitanguliwa na uchaguzi wa Halmashauri ya
Wachaga wote kuanzia kwenye ngazi ya Uchili
(kijiji), Umangi ( uchifu wa eneo) na mwisho
ngazi ya baraza kuu.
Sherehe ziliadhimishwa mjini Moshi ambako
Wachaga wote pamoja na wageni waalikwa
kutoka mataifa mbalimbali walikusanyika katika
Viwanja vya Halmashauri ya Uchaga (sasa ni
makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya
Moshi, [Kilimanjaro District Council-KDC])
kushuhudia sherehe kubwa na yenye kusisimua
sana.
Jumba la Makumbusho
Upo umuhimu mkubwa wa kuhifadhi historia ya
Wachaga kama kumbukumbu sahihi kwa vizazi
vya sasa na vijavyo.
MWISHO.
PUNGUZA MANYAMA UZEMBE....
NO MORE MANYAMA UZEMBE!!!!!!!!
*****KWA DAWA ZA KUPUNGUZA TUMBO NA MANYAMA UZEMBE WASILIANA NA FETTY KWA SIMU NAMBA +255 767 728 764*****
Utatumiwa Popote Ulipo, Just call/ WhatsApp Or Sms +255 767 728 764
Matangazo
Kwa Matangazo Wasiliana Nasi Kwa 0753 891 997
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
NGUVU DRINK
NGUVU = Nguvu Zaidi Ni Spirit Drink INGREDIENTS: Fine spirit, Gin flavour & Ionised water "Not For Sale To Person Under The Age Of 18" P.o.Box 54280, Dar es salaam,Tanzania
NGUVU SPIRIT AVAILABLE AT GF MIN-DEPOT
No comments:
Post a Comment