PUNGUZA MANYAMA UZEMBE....

NO MORE MANYAMA UZEMBE!!!!!!!!
*****KWA DAWA ZA KUPUNGUZA TUMBO NA MANYAMA UZEMBE WASILIANA NA FETTY KWA SIMU NAMBA +255 767 728 764*****
Utatumiwa Popote Ulipo, Just call/ WhatsApp Or Sms +255 767 728 764

Matangazo

Kwa Matangazo Wasiliana Nasi Kwa 0753 891 997

Friday, April 10, 2015

HAPA NILICHEMKA SANA AISEEE... HAHAHAAA

Hello beautiful peoples,
I love Fridays sana... Thanx God its Friday, furahaa day!!

Sasa leo kwa wale wanaosemaga mie napenda kujisifia sana wawe attention... Leo ni kujiponda tuu...
Ila kweli ni kwamba mie ni muongeaji sana so ukiona naongea kujisifia ujue vipo vya kujisifia maana siwezi kuongea tuu vitu visivyokuwepo... Sasa leo vipo vya kujiponda na ndio naanza ivo kujiponda kama ifuatavyo....

Nasemaga in fashion worlds you should break all the rules ila hapa aisee nilichemka... Some rules were not meant to be broken kabisaaaaaaaaaa!!!
Eti na mie nilinunua jumpsuit (I bought it through Instagram) yaani ilivyokuwa amevalishwa mdoli nilidata nayo... i loved it hatareee... And it was expensive, dears...when i say expensive aisee muelewe yaani it was very expensive... Ila niliona it worth it,ukizingatia sipatagi size za jump-suit nzuri, hii ilikuwa ya kwanza kuipenda and ni size ya kibonge so kwa picha tuu nilidata...

Nilishauriwa sana nisiinunue na kila mtu niliekuwa namuambia i need this jump-suit, ila kiherehere changu tuu na mie niwe nimevaa jumpsuit jamaniiii...

Kweli kwa masifa i did the procedures za kuinunua, they were so sweet yaani nilifurahia kufanya nao biashara then nikawapa address yangu wakanitumia, it's realy nice and quality.. 
Ila tuuuuu hakutakiwa kuivaa mtu kama mie.. Yaani hii ni ya mtu mfupi and mnene, tena huo unene wake huyo mtu uwe unene wa kueleweka kiuno kipo wapi na pia awe na hagger(makalio) la uhakika ndio atapendeza.. Mie na hii pasi yangu ya kichagga hapo siwezi hata kugeuka, hahahahaaaaaa!!!! Maana ni kitu cha flat-screen (In Faith's voice) Hahahahahaaaa....
Na kama akiwa mrefu basi awe na mguu chupa ya bia, sio toothpicks za kichagga kama izo zangu apo... 

Pia awe na kifua cha wastani, ikiwezekana awe hajanyonyesha kabisaaaa
(Ila kama amenyonyesha awe na bra zenye viwango to boost up matiti yake) Maana si mnaona uwazi wa mbele na nyuma ulivyo matata....

Mmmmh, sijapendeza aiseee... Uuuuuwiii, hii itakuwa post ya kwanza kuifuta siku nikiamua kuanza kufuta post huku... Dah!!!


Nimeshaivaa hii jump-suit twice na mara zote niliiva in mitoko ya usiku na ukweli sijawahi jipenda nikiivaa, hadi leo ipo kabatini for more than a year na bado naiwazia pose la kuivaa sipati picha...

Sasa nimeamua tuu kuigawa hii jumpsuit, kama una vigezo wewe nicheck wassap 0753 891 997.. Naigawa bure kabisa kwa atakayekuwa interested nayo pia awe na vigezo, hata ukiwa nje ya Iringa nitakutumia ulipo, you just check me kama una vigezo..


I would love pia ikikufikia uivae then ujipige picha na mie nikuone kama umeitendea haki hii jump-suit maana jamaniii ni niliinunua  ghaliiii, uuuwiiiiii... Hapa ninavyoigawa roho inaniuma ni vile tuu nawapenda sana wasomaji wa hii blog, na ikimpata mtu mwenye vigezo aiseee nitafurahi maana nitaona hela yangu haikwenda bure... Sawa eeeh???!!! 



Nice week-end dears,
XOXO!!!

3 comments:

NGUVU DRINK

NGUVU = Nguvu Zaidi Ni Spirit Drink INGREDIENTS: Fine spirit, Gin flavour & Ionised water "Not For Sale To Person Under The Age Of 18" P.o.Box 54280, Dar es salaam,Tanzania

NGUVU SPIRIT AVAILABLE AT GF MIN-DEPOT