Chibu Dangote wa Tz a.k.a Diamond  Kumtoa Wema Kimataifa!
“Hapa juzi kati kulikuwa na mazungumzo, kuna mtu mmoja anaitwa Frank 
yupo huko Ghana, ni mtu mkubwa sana, na yeye ndio anaandaaga zile tuzo 
za Ghana, kwasababu kuna movie anataka kuifanya baby. Hiyo movie wajue 
kabisa eeh Sepetunga kaachia mashine mpya. So jamaa yule ana link na 
watu wengi nikajaribu kuzungumza kuwapata actors na actress ambao 
anaweza kushirikiana nao kwa sababu namna pekee ya kuweza kutanua market
 yako katika kazi yoyote ni kushirikiana na mtu ambae yupo katika nchi 
nyingine ili kuweza wewe kupenyeza bidhaa yako wewe na yeye apenyeze 
bidhaa yake kwako,” alisema Diamond.
Bado Diamond hajamaliza, akaendelea....
“Kama akina Van Vicker sijui akina nani, nimefanya mazungumzo nao 
kuangalia namna gani wanaweza kufanya movie na movie ifanyike Tanzania 
au ifanyike Nigeria au ifanyike Ghana. Ghana, Nigeria ni nchi ambazo 
zina nguvu kwenye soko la movie Afrika. Wakati nazungumza nao pia uzuri 
ilikuwa ni rahisi hivi baby kamlink sehemu yoyote ni rahisi sana kwa 
sababu kwanza ana content nyingi za movie zake. CV zake ni rahisi 
kumwambia mtu hiki na hiki, kwahiyo mtu akiona anashtuka, yaani mtu 
anakuwa excited kufanya naye kitu. So na wao pia kuna movie wanataka 
ashiriki uzuri pia wakasifika Kiingereza chake ni rahisi zaidi kufanya 
naye kazi. Kwahiyo mwenyezi Mungu akisaidia kuna mipango itakaa sawa 
basi mwaka huu utakuwa ni mwaka wake mzuri na zaidi nafikiri hata kabla 
hata mwaka haujaisha hii project itakuwa imekamilika labda inaweza kuwa 
out sijui yeye ndiyo anajua zaidi lakini. Wajibu wangu ni kutekeleza 
kuona kwamba baby amefanya movie na fulani na fulani kutoka nchi fulani 
na movie imekuwa fulani na kulingana alivyokuwa mwanzo na sasa hivi 
aonekane ame advance kutoka pale alipokuwa mwanzo.”
All the best Mr & Mrs Tanzania.... Kisses back!!!!
  
 
 
 

 
 
 
 
Asante chibu
ReplyDelete