Hiki Ndicho Alikiandika Flora Mbasha Jana
"Kama unaweza kushiriki maombi haya pamoja nami, Mungu akukumbuke, na
kama upo kwa ajili ya kuhukumu, pia Mungu akukumbuke. Math7:1 Msihukumu
msije mkahukumiwa ninyi, kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayo
hukumuwa; na kipimo kile mpimiacho ndicho mtakacho pimiwa.
Math5:44 Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.
‘ Mungu wewe ni Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. wewe ni Mkuu sana, wewe
ni mwanzo tena mwisho zaidi yako hakuna na hatakuwepo. umesema ktk
1wathesalonike5:18 shukuruni kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi ya
Mungu kwenu ktk kristo Yesu. ahsante Mungu maana wewe uliijua jana
yangu, leo na kesho itakuwaje.Mungu wa amani unitakase kabisa nafsi
yangu, mwili wangu na roho yangu unihifadhi, wewe BWANA ni mwaminifu.
Ktk Isaya43;19 umesema,Tazama nitatenda neno jipya: sasa litachipuka je
hamtalijua sasa? nitafanya njia hata jangwani na miito ya maji nyikani.
BWANA mapenzi yako yatimizwe, tenda lililo kusudi lako juu yangu. ktk
Math14:14 umesema, mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya.
ukasema ktk Marko10:27 Yesu akawakazia macho akasema, kwa wanadamu
haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo: maana yote yanawezekana kwa Mungu.
Maombolezo3:31-32 Kwa kuwa BWANA hatamtupa mtu hata milele, maana ajapo
mhuzunisha atamrehemu kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
Mungu inua moyo wangu sasa, wewe ndiyo msaada pekee wa kweli. Ninaamini
utatenda makuu kama ilivyoandikwa ktk Zaburi 108;13 Kwa msaada wa Mungu
tutatenda makuu, maana yeye atawakanyaga watesi wetu. Bwana wewe ni mtu
wa vita, Bwana ndilo jina lako,pigana sasa ninakuachia wewe.
ninashuka mbele zako ninaungana na wenye uhai wanne ktk Ufunuo4;6-11
kukuabudu wewe nikisema, 11 Umestahili wewe BWANA wetu na MUNGU
wetu,kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwwe
uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako navyo
vikaumbwa.
Zab23;4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami"
AMEN
Duuuu very sad
ReplyDeletejamani.. huruma kweli ila na yeye alizidi kugawa ka pipi
ReplyDeleteAmen
ReplyDelete