PUNGUZA MANYAMA UZEMBE....

NO MORE MANYAMA UZEMBE!!!!!!!!
*****KWA DAWA ZA KUPUNGUZA TUMBO NA MANYAMA UZEMBE WASILIANA NA FETTY KWA SIMU NAMBA +255 767 728 764*****
Utatumiwa Popote Ulipo, Just call/ WhatsApp Or Sms +255 767 728 764

Matangazo

Kwa Matangazo Wasiliana Nasi Kwa 0753 891 997

Friday, February 6, 2015

MAJANGA YA ''HOUSE-GIRL'' WANGU JAMANIIIIII...

Hey darlings...
Habari za siku nyingi??? I realy miss you guys so much!!! Good thing is I am back from our ''road trip''... Yeah, nimerudi!!
 
Wapendwa, yaani I was so anxious kuwaadithia all about trip immediately nilivyofika tuu Iringa but kulitokea majanga ambayo yalini'keep hoi, my brain stucked and mwili mzima ulikuwa kimya hadi jana ndio nimepata nguvu upya...

Yaani kila nikiyafikiria haya majanga natamani like nisingerudi this week, ningekaa zangu tuu nile maisha na wanangu na mume wangu till next week may be ningeweza ku'skip majanga haya...

All is well now, so I can talk about it ili kwa wale walio na watoto wadogo and wanawaamini ma'house girls wao, tena wanawapenda na kuwajali kama ndugu zao pleaseeeeee muache mara moja aiseee, wadada wa kazi sio watu, yaani sio binadamu kabisa hawa wadada.. Ni kama wamezaliwa na mama mmoja sijui..maana siku zote nilikuwaga nasomaga  na kuadisiwa tuu ma'story ya wadada wa kazi kuwatesa watoto (Like yule wa Uganda) ila this time, yamenikuta.....

Tena nilikuwa najipa moyo kuwa wanagu mie wameshakuwa wakubwa so hawawezi kuteswa maana wataniambia, kumbe nilikuwa najidanganya!!!

Nikawa nam'treat house'girl kama mdogo wangu.. Yeyote anayenijua ni shahidi vile ninavyoishi na msichana wa kazi.. Ni zaidi ya rafiki, zaidi ya ndugu, maana naamini ndie anaenisaidia kulea wanangu pamoja na kazi ndogondogo za nyumbani ilaaaa duh!!! Kumbe house'girl alikuwaga anani igizia bongo movie...

Nilikuwa nikiona wadada wa kazi wanateswa nakuwa wa kwanza kuwatetea.. Tena na maneno kibao ya kumponda huyo anayewanyanyasa ila sasa dah!!! Nadhani nitakuwa mmoja wao aisee....
Maana baada ya haya yaliyonitokea, if and only if ningemkamata house'girl wangu nahisi now ningekuwa magereza for murder case au pengine ningemng'atang'ata mwili mzima....

Kwa sasa aisee sidhani kama nitakaa tena na house'girl hivi karibuni, maana nimekoma na nimechoshwa nao.. Hata nanny camera naona haitanisaidia.. Labda kama kungekuwaga na Robort unaloliacha na watoto and mdada ili likiona tuu mdada anamtesa mtoto lina'react hapo hapo linampa kipigo...apo ningetamani mdada wa kazi, ila kwa sasa nooooo!!!! tena BIG NO....

Nitafanya kazi zangu zote by myself na wanangu nitawalea mwenyewe na day care tuu,itanitosha..
Na hata kama ikitokea nakuwa na house'girl tena, nitam'treat as a maid and not ndugu wala rafiki...she'll be a maid and nothing more.. Mshahara nitamlipa tuliokubaliana, hatapata hata extra sh moja from me, yaaniiii naona sasa hivyo ndio watakuwa wanajua kutofautisha kati ya msalaba na kujumlisha... 

Ni majanga yapi hayo yaliyonikuta???
Tulirudi from our safari Monday usiku, kwa vile tulikuwa tumechoka sana, jumanne nilitamani tulale tuu wote but Fred (my son) alikuwa na exams so ilibidi aende shule, Fred (my hubby) nae alisema yupo pouwa so akaenda job, tukabakia mimi, Faith and mdada..
Mida ya saa tatu na mie nikaona bora niende nikaangalie how biashara goes, tena ukizingatia sikuwepo few days... so nikatoka nikamuacha Faith kalala tuu na dada nae yupo anakunywa chai.. 
Ni kawaida yangu kuwajulia hali nyumbani mara kwa mara, mostly when nikiwa nimemuacha mtoto nyumbani, so nilivyofika depot tuu nilimpigia dada nikamuuliza kama Faith ameshaamka,alisema kaamka ndio anakunywa chai..nikaona nisimsumbue anakula nikasema pouwa, mie nikaendelea na mambo yangu... Mchana nikampigia tena dada kumuulizia wanaendeleaje, akasema wapo poa ila Faith kalala, nikasema oky...nikahisi bado ni uchovu wa safari ndio maana kalala mapema, maana Faith hulalaga tena jioni saa kumi.. Ila sikushangaa kwanini kawahi kulala maana dada kashanihakikishia yupo poa, Mchagga nikawa busy nasaka pesa atiii!!

Saa kumi kama na dakika 20 nikapigiwa simu na mlinzi, akaniambia ''njoo haraka mwanao kaumia'' nilishtuka ila sio sanaaa, nikauliza ''kaumia na nini??" ''wapi??" akasema ''kajikata,mguuni'' nikasema ''poa nakuja''
Faster nikawasha gari nikaanza kurudi home, sikuwa na hofu sana maana kila nikijaribu kumpigia mdada alikuwa anaongea na simu nyingine, yaani yupo busy, so nikawa najipa moyo, hadi anaongea na simu haitakuwa serious banaaa....

Ninavyofika tuu, na Fred (my son) nae anashuka kwenye school bus so tukaingia wote ndani...
Uuuuuuwiiii..... hamuwezi amini ni nini nilikutana nacho, nilianza kukutana na damu from mlangoni, kwenye zulia, kwenye makochi kote pamejaa damu.. Mlinzi yupo kam'beba Faith huku mguu kauficha, nika'panic... Nikamwambia mgeuze huku, nipe mwanangu nim'bebe.. mlinzi anakataa ananiambia wewe twende ukawashe gari tumpeleke hospital kwanza, hapo Faith hata halii, kalegea sana na ananiangalia tuu... 
No way, nikapata nguvu ya ajabu, nikamrukia mlinzi na kumnyang'anya Faith, nikamfungua nione alipoumia....
 
 Hii picha ni siku mbili baada ya tukio...

Nilijikuta napiga yoweeee, sijawahi lisikiaga mahali... Nililia kwa sauti hadi majirani wakaanza kuja mmoja mmoja, niliishiwa nguvu nikaanguka chini (ila sikuzimia) Fred (my son) akaanza nae kulia huku ananinyanyua, majirani wakafika, wakijua kuna msiba... Na wengine walikuwa wanauliza ''what is happening in this house??"
Maana wamekuwa wakisikia tuu vilio from mchana hadi usiku...
 
Haukua msiba, ila ni majanga ambayo house'girl wangu alimfanyia mwanangu...
Ngozi yote ya mguu kwa mbele kuanzia chini ya goti ilikuwa imening'inia... Faith kalowa damu hatareee...kalegea hajiwezi... nilimbeba, hapo natetemeka siwezi hata kupaangalia maana panatisha... 
Jirani alinisaidia tukamuwahisha hospital maana hata gari sikuweza endesha, nilikuwa napiga tuu yowe na kulia, manesi walinifunga kanga tumboni (eti walisema inasaidia kupunguza machungu).. Doctor alitaka PF3 wakati anaendelea kumuhudumia Faith maana maelezo niliyompa ya kuumia Faith hayakumridhisha, nilimwambia sijui chochote na kwa muda huo hata PF3 sikuweza kufata maana nilikuwa hoi, alipewa huduma ya faster maana alikua kapoteza damu nyingi sana and finaly alishonwa nyuzi 11...
Yote hayo yanaendelea nikiwa nashuhudia, maana sikutaka kuwa mbali na Faith hata kwa sekunde sifuri.... Hapo mie mwenyewe nipo na drip maana pressure yangu ilipanda sana...
(Tufupishe story sasa nisije nikaanza kulia hapa....)
 *************
Kurudi nyumbani sasa ndio majanga zaidi, that time nilivyokuja kumbuka niliishia tuu sitting room... Sasa chumbani kwangu ndio balaaa, damu zilitapakaa kitanda kizima, chumbani kwa kina Faith pia full damu, jikoni damu kidogo na bafuni pia...

Na mdada wangu alitoroka, hakuwepo yeye wala dalili zake, hapatikani hadi leo.. Kwao hayupo na hakuna anayejua alipo..
Hatuna uhakika ni nini kimempata Faith maana yeye anasema dada alimkata na sahani, sioni hata sahani yenye ncha kali ivo ya kumkata.. Sikuona hata dalili za kuwa na sahani iliyovunjika ndani wala jalalani...
Bado sijui mwanagu alikatwa na nini na kwa sababu gani...
 *******
Majirani walisema wao walianza kusikia Faith akilia tokea saa saba na nusu hiviii, then akanyamaza, akalia tena sana mida ya saa tisa kasoro, alafu akanyamaza, mwishoni ndio alilia hadi akatoka nje mlinzi akamuona hiyo mida ya saa kumi!!
Muda wote huo anaolia alikuwa ndani na mdada according to mlinzi, tena mlinzi yupo very sure kuwa mdada hakutoka kabisa ndani so hatujui kapotelea wapi?? Kiruuuu....
Majirani zangu sio wa'Tanzania so nahisi walikuwa wanaogopa kuingia kuulizia kulikoni??? Maana sie wa'bongo hatuwezi vumilia kilio cha muda mrefu ivo aiseee...tena mtoto mdogo, Uuuuuwiiii.... walisema eti they were trying to call police station for help, hahahaaa...
 
It was such a bad experience... yaani ninavyoelezea sioni kama mnaweza kuelewa what I went through... I went through hell kabisaaa, nikiwaza mdada tulivyokuwa tunaishi nae vizuri, kweli angeweza kumkata mwanangu??? Kwanini lakini??? 

Bado najiuliza sipati majibu, kwani alimkosea nini hicho hadi akaona adhabu pekee ya kumpa ni kumkata???




Namshukuru Mungu, maana alikuwepo kumlinda mwanangu, na alilokuwa amelikusudia Ibilisi limeshindwa kwa Jina la Yesu!!!

That's how Fashionista is... Smile during hard times!!




Nina maswali mengi sana natamani huyo mdada angepatikana hata anijibu machache, ila yote sasa namuachia Mungu... Ila mdada wa kazi mie kwa sasa, uuuuwiii... sijui aisee!!!


Majanga yalitokea Tuesday, niliishiwa nguvu jumatano yote yaani.. Thursday ndio nimepata nguvu ya kumpiga picha na picha nyingine ni za leo...


Leo anaendelea vizuri kabisaa, hadi anatembea mwenyewe japo kwa kuchechemea ila all is well...

Yaani hii post was supposed kuwa post ya kuwaadisia how much We enjoyed kwenye trip yetu, maana we had so so soooo much fun, ila kwasababu ya lijitu lenye roho ya kinyama yaani imebidi nianze kuwaelezea kwanza majangazzz ya house girl...

Msijali lakini... Now tupo oky, nyumbani its only me, my hubby and my F-babies.. Na mie ndio their everything... Mie ndio maid wao, mama yao, mke, mlezi, dobi, mpishi, shoe shiner, msusi na kila kitu yaani.. And you know what, I enjoy maana nakuwa na amani moyoni na uhakika 100% kuwa my kids wapo in safe hands!!

Nikitoka, natoka nao, after school tupo wote yaani full kubanana nao maana they are my everything!!!


Msisitizo jamani, wadada wa kazi sio wa kuwaamini, kuwajali, kuwathamini wala kuwapenda maana machungu wanayokuacha nayo ni bora tuu umtese ata akija kukutenda usipate pressure kama mie... Hahahahaa!!!

This is official yaani #NoMercy to the house'girl# Haki zake nitampa zote ila wema na ukarimu wangu atakaa aupate hata siku moja!!


Ivo ndivyo nilivyoamua kuwa sasa...
 Maana this time wamenigusa at a very sensitive nerve!!

XOXO!!!

4 comments:

NGUVU DRINK

NGUVU = Nguvu Zaidi Ni Spirit Drink INGREDIENTS: Fine spirit, Gin flavour & Ionised water "Not For Sale To Person Under The Age Of 18" P.o.Box 54280, Dar es salaam,Tanzania

NGUVU SPIRIT AVAILABLE AT GF MIN-DEPOT