Hey all,
It's feels so good to be here again...Baada ya kimya kingiii chenye mshindo mkuu, i am back...kibabe kabisa!!!!
And leo it's all about Eve's engagement party... Yes dears,my Eve is officially engaged... and pia she is a bride to be so nipo mkao wa kula mie...(diet i am very sorry kwa muda)
Ila wapendwa wangu, Eve anapenda a private life so i'll do my best ili nisipatwe na mnuno wa mwendokasi... Ila she knows how dada'ake napenda kujishauaaa,lol... so nahisi nikizidisha atanisamehe tuu bure.. Ame vepeee??!!
Nianze kwanza kwa kutoa shukurani zangu za dhati kwa Mungu baba kwa kunipa wadogo wanaojielewa... maana kwa mashauzi haya wallah kuna waja wangeshani'mangeKimambi ila inshallah bado napetaaaa!!! Papa-God thank you oooh...
Pili nimshukuru mnooo Eve kwa kunielewa excuse yangu ya kushindwa kuhudhuria shughuli yake hii muhimu...kimwili sikuwa nae ila kiroho tulikuwa pamoja sana dear....
Tatu na mwisho naomba niwashukuru nyie woteeee, ambao mpo hapa na ambao mlikuwa mnachungulia huku daily kuona kama kuna new posts... Mungu wangu wa mbinguni awape haja za mioyo yenu...m'barikiwe sana wapendwa!!!
Baada ya shukrani sasa ni mwendo wa kujishaua, so naomba tuu kiroho safi kama leo upo out of mood tukutane tena kesho... Ila kama upo na stress-free mood ebu endelea kuwepo tujipe marahaaaa... Maana sitaki kesho tupishane na sura za ''utajijuuu''
Jamani naanza kufanya makusudi mie...naanza mashauzi yangu ya kistaarabu kabisaaaaaa maana hapo sikuhudhuria, ningeudhuria wallah mngenigawa bureeeeeeee!!!!
Ni ukweli wa waziwazi jamani nowdays ku-bebwabebwa kumekuwa habari ya mujini...yaani watu wanabebana tuu kama vifurushi vya taka, hakuna cha mahari wala cha kujionyesha mbele ya wazazi so ukimpata mtu akakuheshimu hadi kuja kukuchukua kwenu kwa heshima na taadhima aiseeee watakiwa kumshukuru mno Mungu...
Na tena sometimes waweza jifikiria na kusema bora hata hao waliopata wa kuwabeba beba...hahahaaa!!!
Unajikuta mtu hadi make-ups zinaanza kudunda usoni, maumivu ya umri yanaonekana waziwazi na hujampata hata wa kukubeba kimya-kimya, si waweza hisi una gundu... So narudia tena jamaniiii ni bahati na ni jambo la kumshukuru Mungu sana kuipata heshima kama aliyoipata Eve wangu...
Maana enzi zetu atleast ndoa zilikuwa nje njeee... Hahahahahaaa, where my age-mates at???!!!! lol
Kuolewa rahaaaa....tena raha sanaaaa, hata uwe bossylady zaidi ya Zari lazima kuna point you'll reach na kutaka uwe na someone to call hubby... Ujishaue na wewe na mumeo...na tena utataka kila mtu ajue una mume...hata awe ''jipu'' viiiiipi, still kuna part of you inayo'feel umuhimu wa yeye kuwepo... So wale ma'independent-ladies wa ''Ooooh mume,mume kitu gani wakati i can manage my life'' Weeeeeee...msiwaamini hata kidogo mwaya, maana hao ndio wapo ready hata kulishwa mavi ili waolewe, japo watoe tuu nuksi nao waitwe ''mke wa mtu'' na kwa wenye mashauzi ndio hao waliopo in the stage ya sizitaki mbichi hizi.... Poleni yenuuuu, endeleeni kumuomba Mungu maana yeye ni wetu sote!!!!
Na piaaaa...Every woman needs a man!!!Period...
So,Eve mpenzi natamani hata nisim'post shem'laa wangu huku maana dada zako ma'single ladies wengine wana technics za kijasusi katika kunyakua nyakua... Hahahahaaa... manyakunyaku mshindweeeee, mniwache mie nijashaue na shem'laa....
Ila nita'post picha zake chacheeee mnooo, till the big-day ndio nitamjaza kila kona ya hii blog... Kwa ruhusa ya wifeyyy to be lakini...lol
Kupendwa napo rahaaaa...
Maana anayekupenda atakuheshimu... Imagne hapo Kishumundu(Manyire) kwetu apo lakini shem'laa hakujali cha mavumbi wala manyasiiii....Kwa ridhaa ya moyo wake akaona to put a ring on it shurtiii goti lipigwe... wallah,he is a keeper!!! Ukimpata mwanaume kama huyu hata ufanye diet mwaka mzimaaaa lazima tuu idunde, so msije mlaumu Eve wangu kumuona ghafla kanifikia... Hahahaaa...
Mjue tuu hizo ni mambo ya mahaba zindekiii... Mahaba from mkata mkaa, hapana chezeiyaaa!!!
Now this is how my Eve looked... She nailed it!!!
Yaani alinoga big time....
Ndani ya Green Max-dress with silver glittered kwa kifua, matched with accessories and shoe...
The very simple make-up na kichina hair-style... In one world yaani ni BEAUTIFUL!!!!!
Dah, mutoto mutamuuu kama wali samaki wa nazi (In kabila la shem'laa voice) hahahahahahaaa....
Sasa mkutane na mpaniaji mwenzangu...yeye nae aliipania shughuli na akawepo... Hahahahaaa, our one and only Doctor wa familia... Doctor Deborah!!!
Yaani ni alinoga as if kaniwakilisha na mie katika mwili wake...ni kama tumevaa pamoja eeee??!!Two in one... mimi na yeye wote, maana huko kupendeza kwake was too big for one person...
Ila JKT nayo shikamoooo... hahahahaa, ka'mwili bado katamu kama cake za Mama T aiseee... Ebu na mie nikazane na diet hadi siku ya wedding my mwili uwe katika mpangilio maalumu.... hahahahahaa!!
Yaani nikiwaga nasema hawa ni wadogo zangu, huwa it feels like i own a BOT wallahiii.... I am one proud dada alive!!!
Wadogo akee mie... Wakiwa na le'bff Janeth wa mie, yaani mlininyooshaaaa...Kila mtu kanoga dadekkkk zangu sasa nitawalipizia siku ya wedding... Uuuuwi, naanza tena kupania..hahahahaa!!!
Hapo sasa ndio a true definition of Beautiful with brain...
Warembo wanaojielewa...
Natamani ni'post picha nyingiiiiiii...ila duh, naombeni nyingine ziwe TBT maana after hii post kuna another post ni muhimu mnooo kuwa posted leo, soooo pleaseee naombeni nimalizie na hizo picha mbili tuu kwa leo atleast Baba na Mama mzaa chema pamoja na dada'Ruth wangu nao wawe wamewakilisha kwa leo... Nawapenda hawa watu zaidi ya vile ninavyojipenda mie... Unaweza mess'up with me na nikakupotezea tuu kiroho safiiii(ila ukizidisha kukupotezea ni ngumu) but you can never mess'up na hao (hata kidunchuuuu tuu) then nikakukalia kimya...That's me, that's my weak-point...My family comes first no matter what....
Eeeh Mungu asante kwa baraka nyingi katika familia yetu...
Stay here, i'll be back shortly...
Love you,
XOXO!!!