Habari zenu, hope wote mpo fine! Mie na familia yangu pia tupo pouwa kabisaaa leo, ila jana jamani I had the worst day of my life... Dah!!! Hadi sikuweza ku'post anything here maana nilikuwa kwenye mapurukushani ya hatareee!!!
Thank God all is well now and am back to my normal routine...
Pata umbea kidunchu about it......
In week days Fred anaenda shule from morning to evening so Faith anakuwa bored ndio maana I decided to take her to the day care from time natoka home mie hadi ninavyorudi I pick her and tunarudi wote home, so nyumbani kwangu hushinda my m'dada and mlinzi...
Sasa Faith had flue, maana haikuwa serious sana nilimpatia tuu Coldril syrup
Timbwili lilianzia hapa.....
Jana morning sasa I noticed she got problems in breathing, sikujali sana coz nilijua ana mafua.. As ussual tukajiandaa zetu ready to hit the road.. In the car nikaona nim'check her nose nione may be pua zimeziba, nimzibue ili aweze kuhema vizuri.. Nilivyomchek sasa... Kiruuuu... Sikutaka kuamini kama ni kitu kipo puani... Nikachukua cotton buds ili nimtoe nikijipa moyo ni makamasi yamemganda.. Ooooh my gosh..si kikazidi kuingia ndani!!!! Macho yamenitoka hapo, natetemeka, namuuliza pua inauma?? anasema eeh inauma kidogo... Natamani nipige makelele nashindwa... namuuliza tena ni nini umeweka puani si akanijibu ''ubuyu''
Guys.... sijui nilipata wapi nguvu za ajabu, niliwasha gari nikaliondoa kama nipo in rally, in zero minute nipo hospital moja Iringa mjini (Siitaji jina please) Nimefika nimemnyanyua Faith mkono mmoja and mwingine nampigia Doctor simu, vile anasema tuu haloo mie tayari nishaingia in his office na kujielezea...
Doctor tried kumtoa for like 20minutes bila mafanikio, usitake kujua hali yangu saa hiyo ilikuwaje maana.. hahahaaa, acha tuu nicheke now!!! maana ungeniona ungehisi I was in labour pain.
Saddly nikaona kama Doctor ananizingua, and zile purukushani za kutolewa Faith akaanza kulia so nikamnyakua faster kwenye gari tena to the next hospital... Mind you hapo sijamwambia mtu yoyote what's going on wala nini.. Yaani nakomaa kivyangu vyangu tuu hapo.. Sijui ndio kuchanganyikiwa au???
To the next hospital napo wakaanza na beat la kumchoma sindano ya maumivu, coz alifika bado analia.. Then shughuli ya kumfanya apige chafya kubwa ikaanza, walifanikiwa kumfanya apige chafya sana ila hakikutoka ng'oo..kilikuwa kikubwa sana.. After chafya nyingi akaanza kutokwa na damu puani.. Wakashauriana wamchome sindano ya usingizi, wakamchoma.. I think walimpa dose ndogo maana hakulala, ila kama 30min hivi alilegea sanaaa.. Damu puani zinazidi kutoka.. Kiruuu!!!!
Napo nikaona wananizingua, nikam'beba mwanangu huyooo, sasa nikaenda Iringa government hospital, dah!!!! Mie nakuwaga mgumu mnoooo kwenda government hospitals jamaniiiii, sio kwa Iringa tuu, even when I was in Arusha, hata nikiwa Mbeya sijawahi waza kabisaaa kwenda government hospital bila kulazimishwa maana nawazaga foleni and other stupid things... Ila kuanzia sasa hii ndio itakuwa hospital yangu.. Sintataka kusikia sijui kwa nani wala wapi tenaaaaa....
Tuendelee sasa na mapurukushani.....
On the way to Iringa gvt hospital sasa my hubby called me tuu kunisalimia, I was like sijui nini, hapo nipo hoi vibaya mnooo... Nikamuelezea shortly what happened and akasema anampigia one doctor nikamuone, I was like oky ila mie ndio kwanza hapo naandikisha daftari la kuingia kwa doctor at gvt hospital.. Hahahaa!!! Mtoto mtamu aisee...
Special appreciations....
Thank you very much Dr.Francis and his wife Mercy, jamani Mungu wa mbinguni awabariki mnoooo, maana walinipa ushirikiano wa hali ya juu..
Tukapewa kitanda and kuandikiwa tuingie theater sasa akafanyiwe operation ndogo atolewe..
Kiukweli ma'nurse pia walinipa moyo sana pale na kunieleza hayo mambo ni ya kawaida kwa watoto and she'll be just fine..
My family is the best family In the whole world....
So nilijitahidi nika'come down to wait for hiyo operation ndogo.. Hapo sasa ndio nikawashirikisha my family, they stopped everything and prayed for Faith...
My mamaa called me and we pray together..
An Angel came from heaven.....
Vile namaliza maombi tuu with my mamaa imagine akaja Doctor mmoja mzee hivi, jina lake nimelisahau ila I heard ni Doctor wa kina mama gvt hospital (naamini alikuwa malaika na alitumwa na Mungu aisee)
Akamshika Faith, akasema this girl is too small for kupigwa ile ganzi ya kuua mwili kabisa theater jamani, ebu nijaribishe old technique if ikishindikana ndio aingie theater... Nilibaki natoa tuu macho hata simuelewi wala sikumjibu chochote.. Maana I was like naomba Mungu tuu huko theater niingie nae..
My God Is A Mirracle working God.....
Yule doctor mzee aliwaita ma'nurse wamsaidie kumshika Faith, yeye alichukua bomba kama mrija, akamuingizia Faith puani upande usio na ''ubuyu'' bomba likaingia like urefu wa kidole cha pete, hapo Faith kashikwa miguu na mikono maana alikuwa analia and kujirusha kwa maumivu anayoyapata.. Then yule doctor akaanza kupuliza lile bomba puani kwa Faith, alilipuliza sana like 3minutes hivi ule ''ubuyu'' upande mwingine wa pua ukatoka puuu.....
I was like AAAAAAAAWWWWWWW..... Nilimrukia yule doctor karibia nimuangushe m'babu wa watu, nilimshukuru yaani...
Faith akawa pouwa kabisaa, damu kutoka puani zikaacha... Akachomwa tuu sindano moja ya maumivu, dawa chache kwa ajili ya kuzuia infections and akapakwa dawa kwa ajili ya bruises...
I am very thankful....
Nilimshukuru Mungu sana and I called my family and hubby kuwajulisha Faith is fine.. And tukarudi zetu home safe and sound!!!
Naamini ni maombi ndio yaliyofanya Faith hakufanyiwa operation ndogo wala nini na ''ubuyu'' ulitoka na Faith yupo salama kabisaa...
Dah...sasa hivi nimemwambia kila mtu yaani sitaki ampe mwanangu ubuyu, pipi wala sijui nini... maana jana ndio niliamini kulea mimba sio kazi, kazi kulea mwana!!!!!
Ushauri kwa wa'mama wengine pia, jamani tuwe tunawachunguza watoto wetu na tuwaelekeze basi wasiwe wanaweka vitu puani, masikioni au hata mdomoni... Jamani mie mwenzenu kwa siku ya jana tuu ni sawa na nimefanya diet ya wiki mbili atiiii.... nimejisikia nime'loose weight sana hadi leo nimeona tuu nipumzike, sijafanya diet kabisaaaaa leo, hapa ninavyoandika nipo zangu Sai Villa napata zangu pizza na milk-shake...Just for today eeh... Kesho naendelea na diet!! Hahahahaaa..
Nawapenda sana!!
XOXO...
Duh pole g. Nimeifatilia iyo stor adi nimesisimka mpnz..mpe pole sana faith pia
ReplyDeleteAsee poleni sana
ReplyDeleteOur God is good.. he is our protector. . Love u my Faith
ReplyDeleteDuh pole g. Nimeifatilia iyo stor adi nimesisimka mpnz..mpe pole sana faith pia
ReplyDeleteMm ningekuwa nimelazwa aisee g u r a strong woman.. polen
ReplyDeleteWangu aliingiza harage sikioni yani nilikaribia kufa c utani..pole sana ndio za watoto izo
ReplyDeletepole sana, ndiio ukubwa huo
ReplyDeleteAsanteni wapenzi wa mie...nimeshapoa mwaya, Mungu yu mwema!!! Nawapenda woteee
ReplyDelete