Yaani kabla sijawaletea hii issue please naombeni mnipe pole...I have to come down kwanza, maana hapa natetemeka kwa hasira, pili nasikitika tukio la kinyama kama hili limetokea at my home city... Eneo ninalolifahamu kabisaaaa... Eeeeeh Mungu, ubaki tuu kuwa Mungu, maana ungekua mimi ningemshika huyo Bwana Rajabu na kumng'oa u'rajabu wake sehemu husika then niuhamishie usoni......
Aya sasa ni nanukuhu.....
"Mtoto
 wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja aliyemtajwa kwa jina moja la Devota 
wa Sokoni One jijini Arusha, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount 
Meru kufuatia kubakwa na njemba mmoja aitwae Rajabu Mkoba (30), mkazi wa
 eneo hilo.Tukio
 hilo lilitokea Jumapili ya Agosti 3, mwaka huu ambapo mtuhumiwa huyo 
anadaiwa kumbaka mtoto huyo kwa saa 9.  
Mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la  
Mwitango alisema siku ya tukio, asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa 
jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga na yeye kwenda 
kwenye kikundi cha akina mama. Usiku saa mbili alikwenda kwa jirani yake huyo kumchukua mtoto wake lakini akaambiwa alichukuliwa na Rajabu. 
“Nilikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, yeye anaishi na wazazi wake. Hata
 hivyo, sikumkuta mwanangu wala mtuhumiwa, nikarejea nyumbani.“Lakini 
kabla sijarudi, nilimwambia mama wa mtuhumiwa kuwa mwanaye kaondoka na 
mtoto wangu akaniambia  nirudi nyumbani nikaendelee kumtafuta nikimkosa 
niende kwake ili akajue cha kufanya, aliamua kwenda polisi’’ alisema 
mwanamke huyo“Ilikuwa saa 9 usiku nikiwa narejea nyumbani kutoka polisi,
 nilimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa akiwa na mtoto wangu akimrejesha 
kwangu lakini mtuhumiwa hakuwepo.“Niliamua kumchunguza vizuri mwanangu 
ndipo nilipogundua kuwa sehemu zake za siri zimevimba kupita kiasi huku 
damu zikimtoka. 
“Nilikwenda kumweleza mama yake jinsi mwanaye alivyomtenda mtoto 
wangu na kumwachia mtoto ampeleke hospitali, alinisihi nisitoe taarifa 
za tukio hilo popote na akaniahidi kunipa shilingi laki moja,” alisema 
mama huyo. 
Imeelezwa kuwa mama wa mtuhumiwa baada ya kukabidhiwa mtoto huyo 
hakumpeleka hospitali badala yake alikuwa akimtibu kwa kutumia miti 
shamba.Baadhi ya majirani walikerwa na kitendo cha mwanamke huyo ambapo 
walimvamia na kumtolea maneno makali ya kumtaka alifikishe suala hilo 
kwenye vyombo vya sheria. 
Kufuatia kelele za majirani ndipo alipokubali kurudi Kituo cha Polisi
 cha Unga Ltd ambapo polisi walifika nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na 
kumchukua mtoto huyo kisha kumwandikia hati ya matibabu (PF3) na 
kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Mount Meru ambako anatibiwa. 
  
Polisi hao walifungua jalada la mashtaka la kubaka na kunajisi lenye 
namba Ung/RB/2473/2014, bado mtuhumiwa hajakamatwa kwani alikimbia baada
 ya tukio hilo lakini mama yake ameshikiliwa kwa mahojiano 
Nimemaliza kunukuhu.... 
|  | 
| Mama pamoja na mtoto aliyebakwa. | 
Pili, wewe kama mzazi after kujua all that, kuwa mwanao kabakwa... kweliiiii, ukakubali kukaa kimya kisa umeahidiwa kupewa laki moja??? Kiruuuu, hata kama maisha magumu huwezi do that to your baby girl jamaniiii.... Au yee mwenzetu hakumzaa??Alishushwa tuu akamdaka???? Maana purukushania za pregnancy hadi kuwa na mtoto wa mwaka mmoja ni sababu tosha ya kuwa na uchungu na mwanao.... Keleuwiiii, ebu huyo mama mzazi kwanza yeye ndio awekwe lock up..... na huyo mama wa mtuhumiwa yeye aachiwe huru maana she is a real mamaa, yupo tayari kumtetea mwanae even if mwanae ni devil...She did nothing wrong, she was playing role ya u'mother apo aisee....
All in all, am mad at that mama mzazi, pili am about to burst kwa hasira nikimuwaza huyo Rajabu.... Ooooh Lord help me, maana ningemshikaaaaaa.... Damn!!!angekielewa kichina in a second!!!! Yaani huu ni ushetani wa hali ya juu..
Eeeh, Mungu mponye huyo mtoto, and pleaseeee dear God, do something to that Rajabu...huko huko alipo atambue kama there is a living God ambaye He doesn't sleep wala hasinzii, all the time He watch over little babies..... Amen!!!
!!!........................!!!
 
 
  
 
Amen
ReplyDeleteJamanii inasikitisha
ReplyDeletemungu wanguuuu
ReplyDelete