Hey all,
Uvumilivu wa kusubiria picha zote ziwe uploaded umenishindaaaa...nimeona tuu nizi'post hizihizi kwanza then hizo nyingine zitakuwaga throw backs... ama vepeee???!!!
Si mnajua tena kwenye ''The Wedding Day'' sie wengine tulikuwa waalikwa eeeh??!! so hapa leo na'post kwa heshima na taadhima tena nazingatia vigezo vyote na masharti bila kuvunja sheria...
So, tuwe pamoja katika ku'enjoy kile ambacho kipo ndani ya uwezo wangu...ukitaka kuviona vingine zaidi nicheck private nikupe namba za Mr & Mrs Peter....
Aya, tunaanzia kanisani sasa....
Hapo bi.arusi wetu before hajaingia church,
Akiwa na mama mdhamini, wanaingia kanisani...
Beautiful...
Picha za wakiwa wanasema ''i do'' zitakuwaga TBT buanaaaa... Au wasiliana na mie private niku'connect kwa wahusika... Hahahahaaaa!!!
(kuzisubiria picha zote nayo yataka moyooo)
I do...
Yes ofcoz apo lazima walisema ''i do'' ndio maana wakatoka wamevalishana pete and cheti cha ndoa pia kileee tukakisoma...
Wakitoka kanisani...
Picha na wazazi wao nje ya Kanisa Katholiki la Parokia ya Burka Arusha mjini...
Na sasa tunaelekea kupiga picha za ukumbusho....
When Jesus say Yessssss.....
Officially Mr & Mrs Peter Masatu!!!!
Mume halali wa mdogo akee mie...
Muke ya Peter katika ubora wake...
Aaaawww... love birds!!!
Wana makusudi hawaaa...lol Kiss la halaliiiii kabsaaa!!!
Haibiwi mtu apoooo....
Na familia yao ya watoto wanne, apo ka'miss last born wao a.k.a Baraka wa my dada Ruth...
Then tukaenda hotelini sasa...
Maharusi wakiingia... Aaaaaw, finally Baraka is here!!! hahahaaa...
Ghafla nikajikuta napewa cheo cha msema chochote (MC) number two... lol
MC number one was Doto, kaka wa bwana arusi...
Kumbuka sasa apo party ilikuwa imeandaliwa kizunguuu, yaani ya faster tuu tule then kila mtu akaendelee na ustaarabu wake... Ila ndio wakajisahau wakampa cheo mswahiliiii...
Mie huyooo, ndio nikawa msema chochoteee... Ama niliwafurahishaaa!!! Party ilinoga almost tukeshe!!!
That's why Eve huwa anasema i always do complicate things... And mie namwambiaga you always do simplify things...hahahahahahaa!!!
So alivyoona nimepewa cheo cha u'M.C apo akasema owky Gf...i am happy you are our M.C but let me give you my simple idea of this party then add your complications kidogo ila inoge... na mie nikamwambia dogo relaxxxxxx!!!
Nikaanza makeke ya kistaarabu pale...Tukafungua kwa sala...Utambulisho kwa pande zote mbili(ya bwana arusi na ya bi arusi) Then tukafungua shampen... na ili iwe ya kipekee basi waalikwa wakakaa na maharusi ndio wakazunguka kugonga cheers na waalikwa....
Palinogajeeeee....
Then ukawa ni muda wa cake...kama kawa maharusi wetu wakakata cakes na kulishana wao... then wadhamini wao... wakafatia wazazi wote.... then waalikwa woteeee pia tukalishwa cake na maharusi...tena waalikwa tumekaa na maharusi ndio wanatufata kutulisha cake.... Hahahahahaa!!! Chezeiyaaa MC wa mwendokasi mie....
Lovely.....
Ukafatia muda wa msosi...
apo sasa u'MC nikauweka kando kidogooo...hahahahaaa, MC number one akaendelea na taratibu nyingine....
Kitu cha plata...msosi wa kijanjaaa!!!
Baada ya msosi sasa ni muda wa zawadi... Chezeiyaaa M.C niliyekuja naratiba zangu zenye chembechembe za uchagga...Hahahahahaa!!! Maana kumbuka apo harusi haikuwa na vikao,kamati wala michango...then wanataka watulishe, watunyweshe then tuondoke kimya kimyaaa...hapana aiseee!!!
Baba wa bwana arusi...baba mkwe a Eve,yaaniii shikamoo ba'mkwe popote ulipo... Ulinitoa kimaso maso MC mie...Maana hadi niliahirisha safari ya kurudi Iringa ili nimpe kampan shemelaa kwenda bank...maana kui'cash cheque nono vile shurtiii uwe na escort pembeni...
Mzee Masatu alidondosha signature kwenye cheque ya milioniiiii........!!!! Duh..nyingiiiii..... Keleuwiiiii!!!!
Mchagga mate yalinidondoka apo nikaanza kuwaza GF MIN DEPOT ARUSHA BRANCH....Kwa cheque ya watu, hahahahahahahahahahahaaaaaaaa!!!! Shemelaa ebu nifikirie buanaaa...sio kwa kunilaza macho huku naiota iyo cheque, nikinywa maji naiona kwenye glass...na zile 0,000,000/= kama zinanipa kizunguzungu kuzihesabuuu...kwani zilikuwa sifuri ngapi vileeee??!! Mie mbona kama zinanipa amani ya roho wakati mgao haujanifikia badooo.....
Mzee Masatu, wewe ni ba'mkwe wangu pia, na vile ulinikaribisha Musoma, naomba nichukue nafasi hii kukuambia kuwa nakuja wiki ijayo...
Usiniandalie samaki maana wale ulionipa juzi bado wamejaa kwenye freezer... Mizigo mizigo pia kwa safari ndefu utanichosha baba'angu...
Mie naomba tuu kikaratasi chenye hayo ma'00,000,000 mengi mengi kikae kwenye wallet hadi nitakaporudi Iringa nijifanyie party ya welcome home....
Asante kwa kunielewa baba!!!
tunaendelea na zawadi....
Zawadi zawadiiii... watu tupo loaded na mahelaaaa!!!!
(ila ba'mkwe,hizi mbwembwe zisikufanye upunguze zile 00,000,000 baba...hizini mambo tuu za sharing is caring baba'angu) Hahahahahahaaaaa....
Tukimtunza bi.arusi wetu.... Tunamuoshea mfedha-fedha...kila agusalo yeye ni pesaaa tuu...kila apitapo apendwe..Eeee ndiwooo,nani hapendi pesa??!! Pesa sabuni ya roho atiii...
Baada ya mazawadi mengiii. mazito mazito sasa ni shukrani na maneno ya mausia...
Unajua mie kwa experience ya kama 5years hivi nimekaa Iringa nimewasoma Wahehe ni watu wanyenyekevu sana... yaani mnooo...ni too much!! M'hehe ata ukimkwaza ila as long as wewe ni mtu potential kwake wallahy atakupigia na magoti....kitu ambacho mwanzoni nilikuwa naona maajabu coz ni tofauti mnooo na Wachagga... aiseee Mchagga ukimkwaza ata kama ni boss wake jiandae kupata shits za maana, vitisho na ubabe wa kiniaje-niajeee chali'anguu(in Arusha people voice)
And ukimfurahisha Muhehe anaweza akakulamba miguu...hahahahaa, ila ukimfurahisha Mchagga anakuwa Muhehe wa kimjini mjini ghafla.... Apo mchagga hadi kaweka mikono kifuani...aiseeee, aiseeee....walijua kumfurahisha hadi uvungu wa moyo wake... apo ame'apreciate mnoooo...
Angekuwa muhehe uyo angeshakuwa anawalamba watu miguu apo, ila kwa vile ni mchagga aiseeee apo ame'show appreciation ile ya grade A plus...
Hahhahahha...Wahehe nawapenda jameni no hard feelings, ni mnanikoshaga tuu mie na unyenyekevu wenu... msije mkanielewa wrong pleaseee!!!
that smile tells everythingggg....
My woman...My everything!!
Aya sasa tukafunga kwa sala na kuwaruhusu waalikwa kuondoka na waliotakapicha za ukumbusho na maharusi pia ruksaaaa....
Too sweet....
Mapicha picha yakaendeleaaaaaaa.....
hadi giza but sie tunaendelea tuu kwa raha zetu
Priceless...
Family over everything...
With our cousins(mother-side) from Kenya...
Watoto wa our big sisy... Linda & Lucky
Aaaaw..with Gf and F-babies!!
Apo wamechokaaa...sasa tukawaruhusu waende zao honeymoon...
Love is beautiful...
Going to the honeymoon like that.... #MoreThanBlessed
Wana mbwembwe hawa nao pia...hahahahaa... apo ni nje tuu!!
Kufika ndani sasa...
My Eve...
My shemelaa... Peter wa Eve wangu mie!!!!
Hahahahaaa... hatimae Peter ndie anampa Eve tunda, duh!!boraaa,maana...hahahaaaaaaa!!!
(Peter nimekumbuka ile screen-shot yako apo..hahahahhahaah!!!)
Inatosha mamaa,tuhamie side hii sasa...(In Peter voice)
Aaaawww...
EVE: Where are you hubby??!!
PETER: Here i am wifey...
Kilichofuata.....
Vingine sasa watoto mkalale na wakubwa tuendeleee... Ama vepeee???!!!
Tukutane kesho tuendelee na mapicha picha...hadi honeymoon iishe wallahy nitakuwa na stock ya picha za kutoshaaaa!!!!
nimesha'catch ma'feelings na mie ngoja nim'hold baba watoto apa...
Till next time,
Let love lead...
XOXO!!!