It's all about Eve's send off party...
Ilikuwa ni party ya kifamilia tuu and few very close friends... Tulimuaga Eve wetu, home kwetu, kijijini kwetu Manyire Arusha...
Naomba niifanye post hii iwe na maneno machacheee as possible, maana nina picha nyingiii and zote natamani nizipost...so nikiweka porojo zangu hapa wallahy hii post itavunja world's records kwa urefu... (sijui kama nitaweza maana nina mengiiii pia ya kuelezea yaani, hahahaaa... nitajitahidi tuu...hakuna namna)
Aya tuanze sasa, kwanza kabisa hii blog post inakujia kwa udhamini munonooo wa shemelaaaa mwenyewe Mr.Peter.. Asante baba kwa kuniwezesha ku'blog nikiwa napulizwa na kiyoyozi moja matata kabisa hapa kwa kando na Apple juice pembeni...Umetisherrrr sana shemelaaa ake mie...
Pili ni kwa wote wasiotaka kuonekana huku msijali maana sintawa'post... kiukweli naheshimu sana privacy ya mtu so nitajitahidi my very best kuwa'post tuu wale waliopo willing...ukijiona kwa bahati mbaya pleaseeee ujue nimepitiwa tuu...
Tatu natamani niwatambulishe kwenu Mr & Mrs Peter to be ila it already feels like kila mtu ameshawajua...so let's skip that na tuanze hiviiiii.......
Party yetu ilikuwa ya ki'coctail flani iviiii very amazing...Yaani uzungu mwingiiii, uswahili ndio usipimeeee...mix apo apo kigita na kichagga then ongezea tena uzungu mwingine...
Wallahy naweza sema so far that was the very bestttt, verry free and verrryyy classic Send off party niliyohudhuria mwaka huu wote...
Maana kila mtu alikuwa free to do vile anapenda ilimradi mambo yaende sawa... And si mnajua home is always the best eee??!! sasa pata picha partyyy la ki'home home... aiseee was the very bestesssstttttttt....
Kabla sijaendelea na ma'picha picha naomba nitoe shukurani zangu za dhati kwa niaba ya my dad and mamaa kwa wote mliohudhuria na kushirikiana nasi kwa namna moja au nyingine kukamilisha party hii...
Tunamshukuru Mungu kwa mema mengi, baraka tele, afya, amani na furaha...
We are very proud of our Eve kwa kututoa kimaso-maso... Pia asanteni our in-laws kwa kutupa heshima kubwa kama hii!!!
Mungu awabariki sana....
Special thanx to our big sisy Hellen, wifi yetu (mama Levina) kwa kusababisha katika suala zima la maakuli/msosi mtamuuuu sana (hasa hasa lile pilao wallahy naombeni course ya kulipika)...
Asante pia big bro Adam kwa kufanikisha swala zima la nyama nyama, wewe ni noumerrrr kakaa!!
Asante da'Ruth wangu, Doctor wa familia a.k.a Dr.Debby and me katika kupendezesha kijijini kwetu...warembaji wa kujitegemea sie!! Hahahahaaa...
Asante sana Sellah for the beautifu l''Mrs Peter To Be'' Cake, all the way from Dar es salaam (Follow her Instagram @didis_creamcake) and Janeth (Follow her Instagram @janjebby) for the nice cake and cup cakes za ki'A-city... Mlitisha sanaaaa wapenzi wangu!!!
Devine make up, asante kwa kutufanya tung'areee kipenzi... Follow her Instagram page @devine_makeup kwa make ups za kijanja ndani ya A.town na mikoa ya karibu...
Asante sana kaka la makaka...
The one and only ''DON'' wa familia, Barnaba wetu for usafiri usio na stress ya petrol, for drinks na mazaga zaga kibao babe...
Ulisababisha vyema pande zile aiseee!!!! Mungu akubariki zaidi ''ze don'' wetu... Ingawaje uliondoka mapema sana kwa sababu za kikazi ila uwepo wako ulisababisha makubwa mnooo kwenda sawa!!! We love you Barnabas wetu!!!
Hayupo single jamaniiii, he is taken and we gonna officialize it soon ila you can follow him on his Insta page @n.a.b.a.s
Hapo Faith kamsaidia my wii kukaba penalt...hahahahahaaaa!!! hataki muchezo na nyakunyakuzzz....
Dah..eti apo ndio najitahidi kufupisha maneno...Kiruuu, ebu sasa karibuni tukaanze shereheee...
Meet our queen of selfie...bibi arusi wetu to be apo aki'take selfies na dad and mamaa before going to her table....
I just fall for this picture, yaani inaongea maneno matamu sanaaaa!!! I call it picha inenayo mema...
Say AMENNNNNN...
Basi wazazi wakamfikisha Eve kwenye meza yake, tukafungua kwa sala, na Eve akajiona mpweke...eti amepwaya kwenye kiti....
Si unajua sie si watu wa mchezo mchezo....Tukampatia bongeee la kampani from Faith, hahahahahaaaaa....
Eve akasema eti yeye na Faith wana mahaba mazito, na anampenda Faith zaidi ya GF anavyompenda, lol..(Apo kweli aliamua kuturubuni) ilaaaa angefurahi zaidi angepata kampan ya jinsia nyingine kwa siku iyo, then Faith yeye ataendelea kubaki moyoni mwake...
Akajua katuwezaaaa...kumbe alisahau sie hatupendi ujinga... Hahahhaahahaha....
Tukamlete wa jinsia nyingine tena wawili kwa mpigo...
Apo ndio akagundua sie sio watu wa mchezo mchezo aiseee... Ikabidi tuu aseme jameniiii mie hapa mbele leo nataka nikae na murume wani... Sasa apo kwa vile wengiiii wetu tulikuwa ni wachagga tukabaki tumetoa tuu macho... Kiruuuu, kumbe kuna mugita mumojaa kutoka pande za Musoma yeye alielewa what Eve alimaanisha... Ghafla Eve huyooo, kumfata m'gita wake, sie tukabaki ''macho kodo-kodooooo tukakodoaaa kodo,tukakodoaaaa''
Kumbe huyooo ndio Murume wani ''in Eve's voice'' hahahahaaaaa.....
Mchagga wa kizungu a.k.a my dad... Mwenyewe hanaga makuu wala hana hiana, akampokea ''murume wani'' wa Eve pamoja na ndugu,jamaa na marafiki wote from our in-laws....Akawakaribisha Manyire kwetu...
(hahahahahahaha,Peter unaninyoosha wallahy maana haya mazingira uliyoniweka ni'blogie ndio yananifanya naongea maneno menggiiiiii wakati mie sitaki...hahahahahaaaa...Chezeiyaaaa ku'blog kwa udhamini munonoooo weye)
Baada ya utambulisho from our in-laws... Na mambo mambo mengine machache yaliendelea then Our sweetes boy Lucky, mtoto wa our big sisy akaomba special chance ya kumpa ma'mdogo wake a very special taji... Alilitengeneze mwenyeweee kwa mikono yake ili amvalishe ma'mdogo Eve...
Too sweet!!!
Apo kila kitu sasa kikawa sauwaaa kabaisaaa....tukaendelea!!Hahahahahahahaa... I wish niwe napost picha zote ila as i said mwanzoni kuwa naheshimu privacy za watu... So najitahidi mnooo kuziweka picha ziendane kimatukio bila kuharibu mpangilio na still watu wengine wasikwazike kwa kuwekwa hapa... Nadhani tunaenda sawa eee?!
Eve naona apo tabasamu likawa kuntuuuu....
Akawapokea wakwe na mu'beibeee kwa kitu cha shampen... Eeeeh, mwanamke shurti ujue kunesa nesa na shampein buanaaaaa....
Pozi apo kama vile Peter anasema Wantekenyaga ukinyongaaa salomeeee, Eve anamaliziaje vilee................................... Eeeeewaaah!!! Ivo ivo mlivyomalizia... Hahahhaaaaa... Ukipendwa ringaaaa!!!!
Doctor nae hakuwepo nyuma katika sualaa zima la kufungua shampen...yaani jamani Doctor that day alifanya kazi nyingiiii,dah...pole mdogo wangu, maana kiukweli hataa hukuonyesha kuchokaaa sana..ila tuu niliamini ulichoka kipenzi haswaaa pale ulipogoma kuvaa hills...hahahahaaa.. Ila nilielewa my dear, and unajua ni neneee???!!! Ulinogaaaa, yaani ulifunikaaa hatareeee kabaisaaa mdogo wa mie...
Doctor mrembo hadi mgonjwa anapona bila matibabu... Hahahahhaaa, doctor akikuangalia tuu na jicho lake weee unapona fastaaa... Jicho jichoooo mutoto...
Ghafla nakufananisha na VeraSadiki...hahahahahaaaa!!!!
Kiruuuu...tuendelee na shampen wapendwa wa mie...
Ikamiminwaaa....
Wakagonga cheerssss....
Wakanyweshanaaaa....
Cheers na wazazi...
Msijali maana nishatanguliza barua ya maombi kwa wazazi wa Peter atleast siku ya wedding waniruhusu ku'post picha yao ya cheers...hahahahaaa... Masharti na vigezo nitavizingatia maana nimeomba kwa heshima na taadhima!!!
Wote tukagonga Cheerssss na wapendwa wetu... Tukawatakia kila lenye heri liwapate na kila ovu liwapitie mbaliiiii!!!!
Baada ya wote kugonga Cheers sasa ni time ya Cake... Yesssss, sekta muhimu iyo..hahahahaaa...
Cake ya kwanza was from the parents, walishindwa kumwambia Eve good-bye... Instead walimwambia wanampenda!!!
And since watoto wetu wanawawakilisha wazazi wetu (As Faith is my mamaa's name-sake so yeye ni mama'angu na Fred since ni first born basi yeye ni baba mkwe na baba'angu apo apo since sina other son...so as applied to watoto wa my sisys n bros) So wao walitoa Cake ya pamoja na wazazi, ''we love u daughter cup-cakes)
Babu,Bibi na wajukuu wakimkabidhi Eve cake and cup-cakes....
Akapokea, akashukuru....
Second cake is from her dadazzzz... Madada wa nguvuuu!!!
Tukamkabidhi Mrs Peter To Be...
Eve akasema yee alimfunza mama kuwa kila atakachopokea ni lazima nae atoe... So akapokea Cakes na akutulisha woteeeee...
From wazazi wote to kila aliyehudhurua....
Naomba tuu niji'post na mie nikila cake then wengine nitawapostigi siku nyingine, ili nijitahidi kumaliza matukio yote fastaaa... Maana juice ya Apple iliisha nikaletewa milk-shake ya vanila, hata sijaimaliza sasa nishaletewa ''plata'' (Mixed nyama za kila aina in one plate) natakiwa nile mie....hahahhahahahaaa... Huu udhamini shemelaaaa, sio wa kitoto...
Aaaaw...ni udhamini munono munooooo!!!!
After cakes sasa ni msosi timeeee....
Dah, hapa ninavyo'blog nalikumbuka lile pilao...Wallahy lilikuwa kuntuuuuu!!! Thanks God nina ''plata'' yangu hapa so mambo yanaenda sawa...
Msosi unaendeleaaaa....
Hahahahahahahaaaaaaa.....ila aliyenipiga mie na wanangu hii picha mungu anamuonaaa... hahahahahahahahaa, sio kwa kuzama hukooo deep in msosiiii...lohhhh!!!! Mcheck ebu Fred apo jamaniiii, hahahahahaaaaa... sijui ni nyama ile mdomoni anaisikilizia apo kama aweke kijiko chini aikule vizuri na mkono,lol..Faith sasaaa hahahahahaaaaa, mdomoni kumejaa bado mkononi kuna nyama, njoo sasa kwa mama la mama..Uuuuuwiii, namtafuta mie aliyenipiga hii picha... Wallahy ana zawadi yake, ebu ajitokeze tuu fasta..hahahaaa...maana sio kwa mimashavu hayooo and kama vile kapilao kameingia kwenye shavu so hapo nakaweka sawa...
hahahahahahahahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!
My ribs....
Baada ya msosi sasa ni zawadi time...
Mamaa akimsomea Eve zawadi zake...
Cheque ya pesa taslim za kiTanzania ambayo ni siri yao na Eve, na Peter nahisi...hahahahaa... Hati ya kiwanja kilichopimwa pamoja na kapu la mama...(Kapu lenye mahitaji muhimu ya nyumbani)
Akashukuru kwa mazawadi yenye uzito munonoooo...
Mambo za madolariiii...
cheko la pesaaaaaaaaaaa hiloooo.....
Mama La Mama nikimtunza mdogo wangu kitu cha kwa obama.... Mie nikitoa pesa za madafu sasa na Faith atoe neneeee???!!! Hahahahaaaa...pata kitu cha Dollar beibyyyy.....
Niongezeeeeeeeeeeee.... hahahahaaa, wallahy nina bitiiii!!!
Apo tena Lucky akaona huyu ma'mdogo ananizoea...mambo za kuvaa na kuvua taji langu sio fresh...sasa namvalisha tena..hahahahaaaaa... Rahaaaaaaaa... Alivyomvalisha tena alafu akamvua na akamvalisha tenaaa...hahahahahahaa
Then zamu ya Faith kutunza....
Mambo za dinner-sets za ukweeeee....
Hahahhaaaa...hapana chazeiyaaa mchagga na pesa aiseeee...yaani kagoma kuziweka dolareee pembeniii... Anapokea nazo zawadi nyingine ivo ivo kazishikilia...hahahahaaa!!! Tisherrr sana dear...
Doctor ulitisherrr mamaaa....
Dah...kiukweli nimejitahidi kuyakumbuka matukio mengiii...hata kama sio yote ila 90% nimeyaelezea apo... Hope mme'enjoy kuwepo hapa leo... Na si mnajua Mungu ni wetu sote eeeeh???!!! So msi'panick kwa baraka za wenzako... endelea kumuomba Mungu na wewe atakujalia... One day yessss, ama nene??!!!
Peter na Eve, tunawaombea kwa Mungu aendelee kuwabariki... mmalize safari yenu hii pamoja na awape watoto kama hao mliopiga nao picha hapo... Hahahahaaaa... Iyo ndio iwe familia yenu, one girl and three boys, hahahahahaaa..Inshallah!!!
Sasa wacha tujishauweeee.....
Hahahahaahahahaaa.... bi.arusi to be ulitishaaaa, itabidi Debby akufundishe mapozi ya ki'bi arusiiii...
maana doctor nae mtataaa..lol
maana doctor nae mtataaa..lol
Meet Gf katika ubora wangu sasa....
Aaaawwww..... Mie and Debby on pointtttttt
Mie na roho zangu....
mapicha-pichaaa kwa kwenda mbeleeey
Naombeni niwaage sasa...
Asanteni wote kwa uwepo wenu...
Tunawapenda sanaaa!!!
XOXO...
No comments:
Post a Comment