PUNGUZA MANYAMA UZEMBE....

NO MORE MANYAMA UZEMBE!!!!!!!!
*****KWA DAWA ZA KUPUNGUZA TUMBO NA MANYAMA UZEMBE WASILIANA NA FETTY KWA SIMU NAMBA +255 767 728 764*****
Utatumiwa Popote Ulipo, Just call/ WhatsApp Or Sms +255 767 728 764

Matangazo

Kwa Matangazo Wasiliana Nasi Kwa 0753 891 997

Saturday, February 28, 2015

ALVIN....

Hi dolls...
Mambo za week'end ni ajee??!!
Mie nipo very oky, busy na life!!
Leo I came across these pics and nikajikuta nam'miss this little boy soooooo much... Alvin I miss youuuu!!!


Alvin is my best friend's(Johary) son...When alivyotutembelea mie nilikuwa naumwa mafua and nakohoa hatareeee... (ndio that time when my mama mkwe sends me her maid kunisaidia) So leo kilichonifanya nim'miss Alvin sana ni nimekumbuka nilivyokuwa nacheza nae nikikohoa anashtukajeee... Hahahahaaa, and akawa bado anapenda tucheze wote, i loved that!!!

Alvin alivyo mtundu sasaaaa... anajifunza kupiga atua so anasimama mwenyewe na meza au anything akikishika anasimama, sasa when he does that anataka kuanguka, mimi ndio nashtuka hadi analia jamaniiiii...
Johary(Alivn's mum & my bestie) akawa ananiambia nisishtuke, so when nikijikaza nisishtuke akawa halii ata akianguka... lol, that's a very good thing to be a baby eeeh???!!!
Eti nikishtuka ndio analia, nikimchunia anakaa kimya anaanza tena kusimama upya.. Hahahahaaaaa... I realy miss you Alvin, I think I need a small baby at my house, yes!!!

Johary, Gf, Alvin & Faith




Mie na Alvin apo na mahaba yetu wala hatuna habareee...


Eeeeh Mungu tukuzie watoto wetu, wakuwe katika maadili mema na afya njema.. AMEN!!



Nawapenda...
XOXO!!!

Wednesday, February 25, 2015

NEW LOOK...

Dears,
Pata muonekano wangu mpya japo kidunchuuuu...







XOXO!!!

MY FIRST BORN IS 5 YEARS OLD... THANK YOU JESUS!!!

Dears,
As my son kufikisha miaka mitano, nina mengi sana ya kumshukuru MUNGU kwa ajili yake..
Lord, I am thankfull!!!
 My first born.. My Fred!!


Five years ago Mungu aliporuhusu nifanyiwe upasuaji kumleta Fred(Son) duniani, shetani alipata njia ya kunijaribu.. Uzazi wangu ukawa na ma'complications kibao...
Nilikuwa na nguvu kabisaa till a week before 23rd Feb 2010 ila nilikuwa na uwoga sana maana kila kilichokuwa kinanitokea was very new to me... Nilikuwa na maumivu ya ajabu for a whole week, maumivu ambayo sio uchungu according to madaktari..(i've never had uchungu)..  Ila nilikuwa na nguvu ya ajabu, nilikuwa naweza kufanya almost kila kitu by myself...nilikuwa sipendi nisaidiwe kitu yaani...
Nilikuwa chini ya uangalizi wa daktari maana makadirio yalikuwa yamepitiliza sana.. Hapo pia mimi niliogopa kidogo maana nilipitiliza months ata sio a week or two.. Na zaidi pia Ultra sound zilionyesha mtoto yupo ready kabisaa kutoka, ila njia ziligoma kufunguka na hazikuwa hata na dalili ya kufunguka kabisaa..
Sikuwa najua lolote about njia kufunguka zaidi ya kuwa tuu nasubiria nione atakavyotoka mtoto..
Wakati nasubiria siku mtoto wangu atoke kumbe nae mtoto akachoka sana na mapigo yake ya moyo yakashuka, my blood pressure shoot and maumivu yaliongezeka.. Nikawa siwezi kupumua vizuri ila najikaza napumua na mdomo, wakaniwekea mashine ya kupulia.. Mwili ukaanza kuvimba... It was a very scary moment aisee....
Iyo sasa ni 23rd Feb 2010 mchana saa nane madaktari walitaka tu'sign ni nani tunachagua ili wayaokoe maisha yake maana it was a situation ya kumuokoa either ''mama'' au ''mtoto''...
(All that time kumbukeni nilikuwa najielewa kabisaa na nina nguvu kiasi yaani ni kwamba ukisikia vipimo vya doctor anavyoelezea na ukiniangalia mimi unaweza ukasema si kweli nipo in that risk)
Ilitakiwa a'sign mtu wa karibu na mie au ni'sign mwenyewe.. (I guess ndio utaratibu wa iyo hosp ulivyokuwa) Kila mtu alitaka niokolewe mimi, my mama mkwe ndio alisema hilo sio swali la kuulizwa maana jibu ni wazi tuu niokolewe mimi... 
My hubby said ni'sign tuu kuokolewa mimi maana tutapata ''mtoto'' mwingine.. It was such a hard time maana nilikuwa tayari madly in-love na my unborn baby boy(Fred).. I was so much in-love yaani hadi sikutaka tutenganishwe na chochote..
Dears, one secrete about me ni kwamba I pray, so that day all I could think of ni kusali tuu.. And nilisali haswaaa... I prayed like never before, nilisali hadi nikafikia stage ya kumvuta Yesu (like physically yaani) nikamshusha hadi tukawa face to face then nikaanza kuzungumza nae.. And aliniahidi kitu kimoja, atanipa familia nzuri PERIOD!!!!
After that, I refused ku'sign kuniokoa mie... Nilikataa maana niliamini hatatokea ''mtoto'' mwingine kama Fred(son) wangu.. Nili'sign wamuokoe ''mtoto'' kwanza then swala la ''mama'' waache MAPENZI YA MUNGU YATIMIZWE... 
Madaktari walisitasita na maamuzi yangu, ila niliendelea kusisitiza kuwa ''mtoto'' atabaki in safe hands of my mama mkwe and hubby plus so many aunties...
And if sintakuwepo arround to see him, i'll always be watching over him in heaven, ila nikibaki mimi my life will be miserable ambavyo hamna mtu angeweza imagine..

Wapendwa, MUNGU ni mwaminifu na ahadi zako sio kama za wanadamu, akikuahidi jambo lazima alitimize.. Aliniahidi atanipa familia nzuri and that what He did!!!
In less than an hour wote ''mama'' na ''mtoto'' tulitoka theater wazima wa afya and tupo hai hadi leo ni miaka mitano imepita tunaendelea kumtukuza Mungu kwa matendo yake makuu anayotutendea!!
Fred(son) is my original soul, he is my first pure love and my first born ambaye siwezi mpata mwingine kama yeye.. Infact he is actually my very first experience of Agape love.. Upendo ule usio na mawaa, i just love him to bits.. He gave me such a lovely experience ya mother-hood... Asante Mungu kwa zawadi hii nisiyoistahili kwa uwezo na nguvu zangu, bali ni kwa Neema tuu na Rehema zako!!
 What else can I say zaidi ya ASANTE YESU... THANK YOU JESUS FOR EVERYTHING!!!
 

Thank You Jesus Kwa Baby Boy Fred,

XOXO!!!

MY SON'S BIRTHDAY DINNER....

Hey everybody!!!
Namshukuru Mungu kwa zawadi ya uzima na afya njema.. 

Nimekuwa busy these few days na kazi za nyumbani plus my offices, etc.. As I told you kuwa sihitaji maid kwa sasa eeeh... so, sina maid yet, na yule nilipewa na my mama mkwe anisaidie pia kashaondoka maana now nipo oky, no more mafua wala kudeka.. Ingawaje my mama mkwe anataka anidekeze bado ila nimegoma, this time is for real... Me and my F-babies na daddy yao tuu mpaka nisahau machungu ya maids ndio nitakuwa comfortable with one!!

By the way na'enjoy sana kuwa their(my kids&hubby) everything... Yeah, nachoka but it worth millions kuwa sure that they are all safe and happy...
(So mkiona sija'post huku mjue nipoje busy with kitchen matters Hahahahaaa....)

Owky....
Monday 23rd Feb was my son's birthday.. Fred wetu amefikisha 5years old... Yaaniii tunazeeka aisee!!!




Nilitamani nikamfanyie ka'small party shuleni kwao but so bad walikuwa ndio wanaanza exams week hii, na hiyo Jumatatu alikuwa na exam mchana, nikaona nisimsumbue na ma'party ambayo sio necessary sana, pia we might do it next years.. Inshalllah!!!
So, we decide to have a simple family dinner at home.. I cooked for my family, msisitizo jamani ni mimi mwenyewe ndio nilipika.. 
 
Hahahaaaa... (utawajua wasiopenda kupika yaani siku wakipika wanataka kila mtu awa'acknoledge)

Basiiii, nikapika chipsi, tambi, bone'less chicken(tandoor) and chachandu, kachumbari and salads...(chezea mpishi mie)

Bila kusahau, birthday haiwezi kunoga bila kukata na kulishana ''cake''... So we had his(Fred=son) choice of cake ''Ben10'' from Mama T's cake delight!!
It was a blast yaani, tulikula na kunywa.. tukapiga story hadi wengine wakalala hapo hapo(sitting room) wakila cake.. Hahahahaaaa!!!


This is all I want my family to be... Always happy, just us!!




 



 HAPPY BIRTHDAY OUR LOVELY SON
FRED

XOXO!!!

Saturday, February 21, 2015

WELCOME TO THE WORLD EZRA....

Hey...
My big-bro amepata a second born.. A new baby boy!!! Ezra...
Congrats wifi'angu wa nguvu.. Congrats bro Julius, now ni baba Double E, Maana first born ni Ester na sasa kaja Ezra.. Good is so good!!!




Ezra..

XOXO!!!

MADAMME DIRECTOR....

Dolls...

''A WOMAN WHO'S HUSTLING, CAN NEVER UNDERSTAND A WOMAN WHO'S HATING'' By GF



 

 



 

 




 
 Ndio hivyo yaani....
XOXO!!

SITE VISITS.....

Helow dears,
How are you all??!!
Nimewa'miss ni ajeee??!! Dah... I had a busy schedule these past three days yaani hadi nikawa nakosa kabisa muda wa ku'blog... Ila you were all in my prayers.. Yes, nawapenda hadi huwa nawaombea.. By the way nyie kuwa hapa mie ni ''another $'' so lazima niwaombee ili muendelee kuwepo.. Ama neneeee!! (In Vj Penny's voice... Heee,nimemmiss Penny..Ivi yupogo???? Mmmmh..)
 
Dears, as mnakumbuka niliwatangaziaga about frames za maduka eeh??? Thank you all for a very positive support and soon zitajaa before hata hazijaisha.. Na wengine wapo willing kunipa kabisa kodi before hazijawa ready, Duh..naogopa mtani'force banaaa.. Ila am honoured kiukweli... Isnt that nice?? Yeah.. You guys are that much nice... 
 
Ndio nipo kwenye last but one stage, kupauwa...yaani bado sijapaua ila ndio my next stage sasa.. 
Back view..
Mungu akisaidia ikiisha mbele basi nyuma pia nitajenga nyumba za kupanga so stay tune!! Hahahaaa...

Soon Mungu akipenda nitapaua and finishing itakuwa ya kishkaji tuu.. (Si mnaelewa kishkaji eeeh, hamna ma'complications sijui ya aluminium na makorokocho expensive, ni simple tuu) Then mtakuwa ready sasa kuanza kunipa mahela...When it's done!!! Ama neneeee... (In my voice)  
So you better wish niwe mama mwenye nyumba wako.. Hahahahaaa!!!

Aya, wale wa kumfikishia Fred (my hubby) what I post here, kwa taarifa yenu hizi picha alinipiga yeye.. Na hapa ninapoandika nipo nae..Hahahahahahhh!!! Huoni aibu sasa???!!! Hahahahaaaaa....
Rahajeee tunavyokuchora,lol... 
Na site huwa naendaga nae most of the time, na akisema kitu nisi'post huwa si'post... Ukiona nime'post basi ujue sijakatazwa.. Na ukiona sija'post pia ujue nimepewa stop... Upo eeeh???
 
Na kama ningekuwaga sikatazwi wallah usingewezaga kuvumilia kunisoma kila siku maana ni sheeeedaaarrrr!!! Hivi tuu vichache roho inakutoka na hukomi bado unarudi kunisoma... Keleuwiiii... If ningeachia kila kitu my dear ndio ningekukera kama vile post za Diamond&Zari zinavyowakera TeamWema.. Hahahahahaaaa!!! Maana sio ndimu tuu hapa, hadi vinegar, masala, mdalasini, mayonise na royco vinapatikana.. Hahahahaaa!!!

All in all, you dont like things I post bora usiwe unanisoma.. Rahisi tuu kiroho safi, you dont view my blog,problem solved.. Ila kama bado unanisoma my kipenzi you like it!!! ''Envy is a new hate'' in Madame Wema's voice!!



Nawapenda.. 
Alafu when I say Nawapenda, huwa namaanisha kweli Nawapenda!!!

XOXO!!!

Tuesday, February 17, 2015

MISS MY BLACK HAIR...

Dolls..
Yaani nimekumbana na hizi picha leo, nahisi sijawahi zi'post eeeh??? 

Duh,nimejikuta ghafla nime'miss my black hair jamaniiiii...
 
Ivi si nilimuahidi mtu kuwa nanyoa?? Hahahaa, akisoma hapa atanikumbushaje leo, uuuuwiiii...
 
Nitanyoa kweli au??? Haahhhahahaahaa.... 
 
Aisee bado naomba nizichezee zaidi... hadi bleach izinyonyoe zote ndio nitaenda salun kunyoa nizimalizie, otherwise leo please niende salun mara ya mwisho mwishoo kuzichezea tena!!!

Nawa'love love woteee...
XOXO!!!

TUESDAY FLANI IVIII....

Dolls..
Haya yalikuwaga mambo ya Tuesday flani ivii amazing #TBT


Mashallah!!!!


Mie..



Do I look pregooo??? Mmmmh...


XOXO!!!

BATA LA VALENTINE ''ZARI & DIAMOND''

Helow dears.... 
Mamboz!!!
Wakati wengine tukiendelea na kula chocklates zetu na ma'nini ma'ninii....huku wenzetu wanakula upepo wa bahari... Hhahahaaaa.. Kweli kupendwa raha, haswaaaa upendwe na yule unayemzimikia kinoma noma, ama neneeee (In Wema's voice)

Hili ndio lilikuwa bata la valentine la ''kaka'' pamoja na wifi yetu lilikuwa Zanzibar
Hadi raha wallah!!!!

 
Yeuwiiii...ivi wataachana kweli hawa??? Hahahahaaa..
Just thinking tuu aisee itakuwa noumer!!!

 
Zari tukomesheeee wifi yetu!!!



Wapi ndimuuuu...maana nazihitaji kwa wingi aiseee.. Hapa nimenunajeeee!!!

XOXO!!!

NGUVU DRINK

NGUVU = Nguvu Zaidi Ni Spirit Drink INGREDIENTS: Fine spirit, Gin flavour & Ionised water "Not For Sale To Person Under The Age Of 18" P.o.Box 54280, Dar es salaam,Tanzania

NGUVU SPIRIT AVAILABLE AT GF MIN-DEPOT