Hope wote mpo pouwa...
Kwanza asanteni sana kwa pole zenu na get well wishes for my baby girl.. Anaendelea vizuri kidogo sasa tunamshukuru Mungu.
Wapenzi, since nilishawaadithia ''majanga'' ya yule house'girl wangu, nimeona sasa niwape ''updates'' ya mambo yalivyoendelea jana..
Basiiii, baada ya ile post ya juzi nilipokea simu,msg,wassap,instamsg na emails nyingi sana za pole,maswali kibao pamoja na ushauri pia... One of the calls ndio imenifanya leo hii niweze kuwapa hii ''update!! Kuna mtu (hataki kutajwa jina) alivyosoma ile post aliniambia yupo tayari kunisaidia tumtafute huyo house girl atleast tuu aweze nipa majibu ya maswali niliyokuwa najiuliza...
Mwanzoni nilikataa na nikaona kama najipotezea muda, ila kiukweli yale maswali ya ''what happened to my baby?'' yalikuwa yakininyima usingizi kabisaaa...
Friday usiku aliniambia nimtumie picha ya huyo house'girl.. Anaitwa Paulina, nikamtumia!!
Aliwaonyesha watu wachache then jana asubuhi akanipigia simu kuwa ameshampata... I was like ''stop kidding na hii issue'' akasema jiandae faster tukamfate...
Kiukweli bado nilikuwa siamini, ila nikasema anyway... kuliko kubaki na maswali yasiyo na majibu ngoja tuu niende, if sio yeye basiiii ila kama ni yeye kitajulikana mbele ya safari...
Nikatoka zangu nikamfata huyo mtu, akaniambia kuna mtu amemwambia kuwa Paulina(huyo house'girl) alimuona tokea juzi kwa jirani yao mmoja ambaye ni dereva fusso.. Huyo dereva ni raia wa Zambia ila ame'rent single room hapa Iringa ili anavyokuwa safarini awe anapata pa kupumzikia..
Mmmmh, nikasema sasa tunaendaje kwa mtu tuu ghafla, nikahisi sio fresh, maana tayari nilishakata RB baada ya Doctor kutaka nipeleke PF3 before dressing day ya kidonda cha Faith, so nilivyoenda kuomba PF3 police walitaka maelezo,niliwapa maelezo kama vile niliwaadithia kuwa sifahamu ni nini kimempata mwanangu maana alikuwa na mdada, nao walitaka wampate huyo mdada ili awaelezee fresh what happened...
So, nikashauri atleast tukatoe taarifa police... Ila je tukifika ikawa sio yeye???
Yule mtu akasema yupo 100% kuwa ndiye yeye..
Tukaenda police, tukajieleza, mie nikasema sina hakika lakini kama ndie mwenyewe, police wakasema hamna shida kama akiwa sio yeye watarudi tuu kituoni ila it's good tukahakikishe..
Safari ikaanza, tukapitaje vichochoroni.. yaani na kukaa kwangu Iringa miaka sijui minne huko sikuwahi fikaga..
Finally tulifika, mimi na yule mtu tukaenda kugonga mlango tulioelekezwa, haukufunguliwa kama five minutes iviii, ila ulikuwa umefungwa kwa ndani that means kuna watu ndani.. Hatukukata tamaa tukasema tukasubirie kidogo then tutakuja kugonga tena.. Ile tunarudi kwenye gari, mlango ukafunguliwa ghafla akatoka mkaka mbiooo... Haaaaa, tulibaki tumeduwaa kwa kweli.. Askari walitaka kumkimbiza ila tuliwaambia sio huyo tunayemtafuta so wakatulia ila waliendelea kuhoji why akimbie???
Mara akatoka Paulina na kanga moja kifuani, hahahaaa... Hapo face to face na mie, alitamani ardhi ipasuke aingie maana pa kukimbia hakupaona, wapo ma'askari watatu, mimi na huyu mtu alietupeleka...
Akaanza kujieleza, hapo hata hatujaongea kitu zaidi ya ma'askari tuu kumkamata na kumwambia avae nguo faster twende kituoni.. Akawa anasema kama ni kwasababu ya Faith yeye hajausika, mara ilikuwa ni bahati mbaya, mara alianguka mwenyewe.. Yaani alitoa kama maelezo kumi tofauti...
Akaendelea...
Kama ni sababu ya huyo aliyekimbia mimi ata simjui, sijui ata anapoishi... Hahahahaa.. (kajisahau kama yupo kwake) hahahaa.. Sijui ndio alichanganyikiwa au???
Basi sasa let's make story short, maana baada ya hapo ''me and her'' had ''our own'' moment kidogo, purukushani za hapa na pale ila aliweza nijibu maswali yangu japo majibu hayakuniridhisha but atleast nilihema *****... !!!!!
Aya... Nilipata hadi nguvu ya kumpiga picha ila si mnajua purukushani za ma'askari, so sikupata picha nzuri sana!!
Hapo ni Central Police - Iringa!
Apo akijiandaa kuingia mahabusu..
There after sasa ndugu zake wakaja kuomba nimsamehe, nifute kesi tuu yaishe.. Binadamu tumeumbiwa makosa na kusameheana ndio maisha mema and blablaaa...
So, nikamsamehe ila tuu awe tayari kunielezea fresh what happened to my girl..
Akasema yupo tayari..
Sasa maelezo yake ndio haya, eti yeye alikuwa anaangalia movie (which nahisi is true, anapendaga sana movie na mie pia that day nilimuacha akinywa chai huku anacheck movie) akamtuma Faith apeleke sahani na vikombe jikoni.. (Imagine hapo Faith hajaenda shule ili apumzike jamaniiii) Faith akakataa, akarudia tena kumtuma nae Faith akakataa tena, ndio akapatwa na mahasira akamnyanyua kwa nguvu akamshikisha vile vyombo na kuanza kum'buruza avipeleke jikoni.. (Chezea mdada wangu anamfundisha binti kazi pamoja na heshima)
So katika kum'buruza vile vyombo vikaanguka vikapasuka, so akaanza kumuuliza kwanini umepasua vyombo??? Apo anamuuliza huku kashika kipande cha sahani iliyopasuka anamnyooshea Faith, eti Faith akaanza kukimbia ndio bahati mbaya akakipitia kile kipande cha sahani chwaaaa nikamchana mguu...
Faith akanzana kulia, akam'bembeleza akanyamaza.. (Nadhani hapo alimchimba biti akae kimya,na ni kweli maana majirani walisema alikuwa analiaaa ananyamaza) Akamfunga na kanga maana damu zilikuwa zinatoka nyingi, ile kanga ikalowa, akamwekea chumvi.. (Uuuuuwiiiii, apo naadisiwa utumbo unanicheza) Alivyowekewa chumvi akalia sana, akaanza fagia vile vyombo faster, kuona Faith bado hanyamazi ndio akaogopa akabeba vyake, na vile vyombo vilivyopasuka akavichanganya na nguo zake maana aliona akienda kuvitupa jalalani mlizi atamuona so akaruka ukuta kwa nyuma akasepa...
Faith alijikata saa saba kwa mujibu wake, yeye aliondoka saa nane na robo... Muda wote huo alikuwa bado anamnyamazisha tuu...
Hiyo ndio story yake....
Nilichoka wapendwa... Ila nimepata nguvu baada ya kujua ukweli.. Sasa I can have another house'girl ilaaaa ataishi kijeshi jeshi kwangu..
*****
Masikini mwanangu, aliteseka mwenyewe from saa nane hadi saa kumi mlinzi anavyomuona.. Nahisi sasa yale maumivu ya chumvi ndio yalimfanya pia azunguke nyumba nzima.. Maana nilikuta damu kila mahali!!Duh, nimemsamehe bure!! Ila alale mahabusu hadi iyo Jumatatu then she is free to go...
******
Asanteni sana wote mlionisaidia kuupata ukweli, asanteni pia kwa maombi yenu na upendo wenu!!
Nimeamini blog yetu sasa inasomwa na wengi, hahahaa!!! Keep it up.. Keep coming here maana sasa I am about kuadisia about safari ileee ilivyokuwa....
More mapicha picha, more mastory and more makila kitu ama neneee...
*******
Kuna mtu alinichekesha eti nikiwa naajiri house'girl niwe naangalia sura, eti sura ngumu ivoo na roho yake ngumu..hahahahaaaa... nimecheka sana, ila nooo bana, iyo sio sababu ya kuwa katili, unaweza pia ukawa mrembo kama mie (msinune maana mie mrembo atiii) na bado ukawa mkatili... Sura haisaidii moyo wako kuwa mwema!!
Wengine wakasema amefanana kabisaa na yule wa Uganda, lol... Hahahahaaaa, apo alivaa shati la yule dereva ndio maana kaonekana hovyo,ila huwaga ni m'poa bana...
******
Have a lovely Sunday my dears,
Nawapenda mno!!
XOXO..
Hahahaaa mbayaaa kama roho yake.. am just glad my Fay ni mzima asee
ReplyDelete