Aya sasa baada ya mikasa na mastory mengi plus ''Debby's week'' and u'busy wa Valentine's day sasa I am all free for you guys...
Hope wote mpo oky, mie bado nadeka tuu na mafua..yaani nimedeka hadi my mama mkwe akaniazima maid wake anisaidie since I told her sina mpango wa kutafuta maid tena... Thank you my hubby's mama..guess you are the best ma'mkwe in the whole world!!
Aya sasa, since hii itakuwa the longest post ever basi tu'skip pictures za ''Official birthday party ya Debby'' pia picha za ''My Valentine's night'' tuziache kwanza, hizo nahisi nitazi'post wiki iyo itakayoanza kesho, right??!
Sasa leo let's see how ''road trip'' yetu ilivyokuwa....
Stay here ili ujue tulienda wapi?? With who?? What did we do?? And so much more.... Ama neneee (In Wema's voice)
DAY 1
Okay my wapenzi, our day one started very early in the morning,ilikuwa kama saa kumi usiku ivii tulipoanza safari yetu.. Tulikuwa mie, my original-soul (Fred=hubby), my first love (Fred=Son) and my shostito wa ukweli (Faith)... Yaani just four of us!! A small circle of real people!!!
Trust me, God is the best driver of all time maana tulifika salama na tulirudi salama...
Aya sasa, by saa moja kasoro tulikuwa tuna-cross Mtera.. Haya maeneo hawaruhusu kupiga picha so nilishindwa kupata picha nzuri.. Ni maeneo wanayotengeneza umeme so hata kusimama pia wanakataa maana wanasema ni maeneo ya hatari.. Thank God maana my F-Babies walikuwa wamelala, maana wangekuwa macho wangeng'ang'aniaje kushuka kushangaa maji yapo chiniii sie tunapita juu!!!
Mtera...
Yaani ndio maana hawaruhusu watu kusimama hapa, maji yanayozalisha umeme ndio yalee na mawaya waya kibao yanapita juu ya barabara... Hatariiii!!!
We had break-fast...
Since kids ndio walikuwa sasa wameamka so it was a perfect time ya kunywa chai and mahanjumati ya asubuhi...
For me, diet ndio ilianza haribikia hapa.. Duh, ma-chapati na maini.... hahahahaa!!! nilijifanya nawalisha watoto ila mwishowe nilikula na mie pia...
Hii restaurant ipo opposite na Maisha Club - Dodoma
Apo ndio Maisha Club, guess one day tutaenda tupaone usiku panakuwaje huko ndani..
Dodoma..
Hatukusimama Singida maana we bought a take away food so tulikula kwenye gari and by that time hubby was tired so I was behind the wheels.. Hapo sasa picha zikawa sio nyingi tena, hahaaaa..poleni!!
By saa kumi na mbili na nusu, wote wamelala (Hubby & F-Babies) na mie nikaanza kusinzia sinzia kidogo wakati tunaipita Mbulu sasa, nikajikaza like one hour nikaanza kukatafuta a nice place ya ku'park ili tupumzike na mie nilale kidogo..
Ile na'park tuu si wakaamka wote, wapo na nguvu mpya na mastor yakaanza.. Hakuna aliyetaka tulale pale so hubby akapokea sterling tukaendelea mara by saa mbili na nusu usiku tukajikuta tupo jijini Arusha, my home my town...
Arusha
Mimi tuu ndiye niliyeonekana kuchoka yaani, wengine wote walikuwa kama ndio wanaanza safari..
Hapo sasa wenyeji wetu wanatusubiria hatareee... Maana walitutegemea tokea saa moja jioni, ila hadi saa tatu bado tulikuwa hatujafika... Tulianza kuzurura jijini Arusha, showing my kids where their mama coming from, where I go to school and bla blazz....
Saa nne nne ivii ndio sasa tukaanza safari yetu ya kwenda home kwetu.. A place called Manyire.. Manyire ni nje ya mji kidogo ya Arusha.. We used kukaa mjini but tokea my dad alivyostaaf walihamia kijijini and nyumba zote za town wamezipangisha.. So Manyire ndio home kwetu..
Tulifika Manyire saa nne na nusu, its like driving ya 30-45min from town to Manyire... Tulipokelewa kwa shangwe hatareeee... Tukashusha mizigo yetu, tukapewa apartment yetu, tukaoga, tukala wali kuku, tukalala..
DAY 2
Yaani siku ya pili tulilala hadi saa tano, tuliamka tuu kwasababu ya njaa... So, immediately tulivyoamka tuu we had heavy breakfast..
Then my hubby wakaenda kuzurura shambani with dad...
Hii ni godawn wanayihifadhia mazao before kuyasafirisha...
F-Babies wakaanza kucheza na Baraka pamoja na kushangaa vitu vya shambani...
Mie nikaanza mastory na my mamaa, nilim'miss jamaniiiiii... Tulipiga mastory mengiiii... Dah, it was such a nice day...
***********
Da'Ruth and her son were there too.. We met Baraka for the first time.. tulifurahi sanaaaa... Tukampa mazawadi yake... Tukam'beba... Dah, Baraka ni bonge la hb yaani... mzurijeee!!!
**********
Eve yeye anaishi mjini, since tuliwaambia pale ndio destination ya safari yetu so atakayetaka kutuona atufate.. So Eve alikuja kutuona, tulifurahi sana.. Tulipiga mastor hadi tukajikuta giza limeingia so Eve nae akabaki home kwa usiku ule....
**********
Aaaaah, nilitaka kusahau aisee about mbuziiii, hahahahaaa... Tulichinjiwa mbuzi, so mkiniona nilivyokuwa kibonge msinilaumu wajameni.....
My son akimuonyesha babu yake kuwa yeye sio muoga, hahahaa!!!
My parents kwa sasa ni wakulima,wafugaji na wafanyabiashara.. Wanalima ndizi, mahindi, maharage, n.k.. Wanafuga mbuzi, kondoo, kuku, bata, ng'ombe na nguruwe.. Pia wananunua mazao from other wakulima na kwenda kuyauza dar-es-salaam...
So walituchinjia huyo mbuzi apo juu...
Tulimla for lunch, choma with ndizi and for dinner wa ku'roast with wali na chips...
Da'Ruth ndiye alikuwa sterring katika swala zima la misosi... Asante my dada maana wote tumekaribia kukufikia sasa.. Hahahaaa!!
Uuuuuwiiiii... tulishiba, hadi nikawa sitamani tena nyama yaani...
DAY 3
Siku ya tatu sasa in kijijini kwetu, eti hii ndio siku na mie nilienda kushangaa mifugo and mazao mashambani... Nilizurura shamba zima more than 50hk yaani nilichoka sana and nilifurahi kuwepo na my family for another day...
Tulianzia hapa karibu na home wamechimba bwawa wanafuga samaki..hawawauzi lakini hawa ni just for fun!! Beach kwetu..hahahaa...
Then tukaenda huku, ni mbali kidogo ndio mabanda ya mifugo.. Wanafuga kisasa so hata mabanda yao wameyajengea kisasa...
My dad and my son, hapo ni mabanda ya nguruwe..
My mamaa ki'shambani zaidi.. Then tukaenda kwenye mabanda ya ng'ombe na mbuzi na kondoo...
Nilikuwa nashindwa kupiga picha nzuri zaidi na nyingi maana apo Faith nimem'beba..anaogopaje hao mifugo sasa.. Hapo hataki hata kushuka chini... Hahahaaa!!
Ila hizi picha chache tuu nadhani mmepata uhondo of what we were doing and see huko kijijini kwetu..
Then tukaenda kuonyweshwa their source of power shambani, kule kwenye nyumba wanatumia umeme wa sollar ila huku kwenye mashamba wanawasha umeme kwa kutumia mbolea(mavi) ya ng'ombe..
And ukipita usiku almost shamba lote lina taa.. Yaani ni kuzuri haswaa..
************
Chuo kipya cha Nelson Mandela kipo jirani kabisaa na kwetu, so baada ya kuzurura shambani siku nzima, jioni tukaenda kuzurura kwenye hiko chuo.. Maana last time I was there ndio kilikuwa kinajengwa jengwa hata hakijaisha fresh ila sasa kimependeza sana, kimekamilika na kimekua kikubwa mno...
Tukashangaa mazingira ya chuo hadi tukachoka...
**********
Debby yeye yupo chuoni KCMC - Moshi, siku hiyo nae alikuwa anakuja kutuona.. So baada ya kumaliza kuzurura chuo cha Nelson Mandela, tulienda kumpokea Debby maeneo ya Tengeru..
Anatupendajeeee... Hahahaaa.. we love her too.. Tulienda kumpokea since kuna distance kidogo from there to home..
So, tulimpokea Debby na mazawadi yake ya kunifanya kibonge.. hahahaaaa!!!
Debby akatupa mastory ya chuo, we were all happy, na ndivyo siku ilivyoisha...
DAY 4
Church day, ilikuwa ni Jumapili... Tulienda kanisani wote.. We had a blessed ibada with my family...
After church...mapicha picha huku nafumua nywele maana zimenichoshaaa.. (Yaani kweli siku hizi sipendi kusuka,duh..hizi nywele nilikaa nazo sijui 5 days tuu nikafumua)
Mchana tukamsindikiza Debby stend ya mabasi ili arudi Moshi...
Debby akijiandaa kurudi chuo... |
Tulienda wote town then Eve alirudi na sisi tena Manyire na jioni ya siku hiyo hiyo tena tulienda kumsalimia my big sisy Hellen and her family since yeye alikuwa na sababu serious ambayo asingeweza kuja kutuona Manyire.. So tulienda kumsalimia maeneo ua Sokon-One Arusha town na kurudi Manyire tena kujiandaa na safari ya kurudi Iringa next day...
DAY 5
Safari ya kurudi Iringa.. Siku hiyo wala hatukuwa na haraka, tulijiandaa mida ya saa moja asubuhi, tukapiga picha za kuagana agana....
We prayed together kumkabidhi Mungu safari yetu tena... And then by saa mbili we hit the road back ti Iringa...
Tuliagana....
Siku iyo ya kurudi my hubby was behind the wheels tokea tunaanza safari hadi tunafika yaani... Kwenye gari we had all we needed so hatukusimama mahali zaidi ya short-calls and to take few pictures!!
By saa moja jioni tulikuwa home sweet home, gangilonga Iringa and We thank God kwa kusafiri salama na kurudi salama!!
The End...
Wote ambao sikuweza kuwaona please mnisamehe bure, next time nitakuja nikae mwezi mzima kabisaaaa...nionane na kila mtu..
Sawa eeeh??!!!
Nawapenda sana, wote wote...
XOXO!!!
nimependa unavyoishi na familia yako
ReplyDeleteMje tena tushawamiss
ReplyDelete