Habari zenu wote.. Hope mpo pouwa as i am!!
Na the big reason ya kufunguka ni baada ya kuamshwa asubuhi asubuhi na kuambiwa nikasome ''facts'' alizoandika Mange huko u-turn blog.... Mnielewe one thing, Mange is one of my role-model, na nampenda sana ila kwa hizi ''facts'' aisee nimeanza kumuangalia na jicho la tatu, haibadilishi kumpenda Mange ila sikubaliani nae kwa hili hata kidogo...
Nimesoma previous post yake kumbe alisema ''atatapika'' and kiukweli that was all she did, ''ametapikaaaaa'' na hajatupa ''facts'' hata moja zaidi ya ''matapishi''...
I expected ma'evidence ila sijaona evidence hata moja zaidi ya kuongelea tuu story tunazozijua kitambo and kutuandikia gazeti reeeeefuuuuuu (I guess that is what she does best)
Issue alizoziongelea katika hizo ''fact'' tano ni yaleyale ya ''richmond'' na ''madawa ya kulevya'' sasa sijui why ali'put five facts wakati was repititions ya ivo vitu viwili tuu...
Kila alichoongea ni marudio ya kila kitu ambacho watanzania woooteeeee tunajua... Nani hajui 'Richmond'??????!!!!! Hadi leo nani hajui kuwa Lowassa ali'resign sababu ya ''richmond"??????? Nani hajui issue ya ''madawa ya kulevya'' kama ni wanasiasa wakubwa ndio wanaohisiwaga enzi na enzi kuwa ndio DrugLords????!!! Issue za madawa ya kulevya kila siku tunaambiwaga kuna mikono ya wanasiasa... Nani hakuwahi kusikia hayo????
Even JK mwenyewe walishasema anawaruhusu wachina waje Tz na walete bidhaa zao kwa sababu mwanae alitaka kunyongwa china kisa madawa ya kulevya so JK akawaomba wasimnyonge and in exchange wachina wapo free kuingia Tz vile wapendavyo... Nani hajawahi sikia hayo?????!!!!
Tumeshayasikia yoooteeee hayo...ni maneno tuu kama ya kwenye kanga maana hatujawahi pewa ''evidence'' hata ya shutuma moja kati ya hizo...
Kwa jinsi tuu ukisoma hizo ''facts'' u-turn, utagundua pia ni maneno yale yaleeeee ya enzi na enzi... Hakuna ''fact'' wala ''evidence'' hapo...
Successful siasa ni kutumia everything possible kuwashawishi watu wakukubali na wakupe madaraka.. Even if it means kuwadanganya, hiyo ndio siasa kama mlikuwa hamjui...
Ila pamoja na mabaya yoooooteee hayo ya wagombea wa CCM jamani LOWASSA is a way better than wagombea woooteee... Yaani LOWASSA ndio chaguo sahihi la mgombea uraisi kwa CCM... Pamoja na u'siasa alio nao pia ana ''utu'' Yesss, Huo ndio ukweli, mpende msipende... Tulieni tuu nitawapa ''facts''!!!
He is a way better maana ali'resign mwenyewe... Haijalishi aliambiwa na JK au vipi, ku'resign inaonyesha ni jinsi gani mtu yupo humble, amefanya kosa (ambalo wewe pia ungelifanya 100%) na ame'pay for it...ameonyesha kujutia na kuachia ngazi... Inahitaji roho ya kipekee sana kujutia kosa lako na ku'take action.. Tena una'take action kwa maamuzi magumuuu...Imagne sehemu unajua kabisa ina hela ndefu alafu unajitoa, hayo ni maamuzi magumu sana, wengine tungeng'ang'ania tuu hadi tuje tutolewe kinguvu, ila yeye alijitoa mwenyewe!!!
Issue ya ''richmond''was terribly bad and ingeweza kumkosesha Lowassa uraisi ila Ku'resign kwa Lowassa tuu yaani mimi hiyo ni sababu toshaaa ya kumchagua awe raisi wa Tanzania...
Sasa facts...
Mimi ni mzaliwa wa Arusha na nimesoma Arusha from baby class hadi University, i guess hapo mnapata picha kuwa naijua Arusha vizuri... Jamani Monduli ndio place iliyoendelea mapema kuliko sehemu zoooteee Arusha, Monduli kuna social services zoooteee tokea enzi mimi nipo primary school... Monduli kuna maji safi kila kona, hospitals, shule kibaooo tena za misaada(yaani unasoma bure) na barabara za mwanzoni kabisa Arusha kuwa na lami ni za Monduli... Hizo zooteee ni juhudi za Lowassa..
''Facts'' kama hizo ndizo zinazofanya umjue nani anafaa kuwa raisi na nani hafai...
Tena nakumbuka nikiwa secondary nilikuwa nahitaji specialist wa macho, Mt.Meru hospital ambayo ndio hospitali ya mkoa nilikosa specialist ila nikampata Monduli... Jamani ukiona sehemu hospital inayo hadi ma'specialists ujue maisha ni mazuri..
Sehemu barabara zina lami hadi vichochoroni, ujue pana maendeleo...
Uliza watu wa Arusha about Lowassa and utapata jibu sahihi kwanini uwanja wa SheikAmri ulifurikaaa... Hamna cha kulipwa wala umbululaaa, watu wa Arusha wanafahamu ni jinsi gani Lowassa alivyowapa maendeleo makubwa... Na ndio maana wataendelea tuu kum'support hataaa iweje....
Ni m'bunge gani alishafanya maendeleo kama Lowassa kwenye jimbo lake?????
Hizi ni zama za ki'digital so wewe iba kula na wenzio na wataku'support 100% maana nao wananufaika na wizi wako... Kuliko hao wanaoiba wanaishia kula na familia zao tuu, majimbo yao yanabaki kuwa masikini wa kutupwaa.... Ulizieni tena vizuriii mpate stori za Monduli na Arusha kiujumla then ndio mtajua kwanini mimi ni Team Lowassa hadi siku mtakayoleta ''fact'' inayoeleweka.... Sio maneno maneno tuu bila evidence, hatutaki maneno, tunataka matendo na Lowassa ameonyesha vitendo so uraisi tutampa maana hata akiiba na sie tutanufaika nae... Tuna imani naye na tunajua maendeleo ya Monduli ataya'spred Tanzania nzima so uraisi tutampaaa.. PERIOD!!!
''Bora mbwa alioshiba kuliko mbwa mwenye njaa'' Akili kichwani mwako....
Sitaki kuingia kwenye siasa na sitaki ''beef'' za kijinga na watu.. Simpigii kampeni mtu ila kama wewe ni mpenda maendeleo utajua ni nani anafaa kuwa rais wetu.. Kama ewe ni mpenda majungu pia utabakia ivo ivo hata Mwl.J.K.Nyerere afufuke akueleweshe siasa za bongo!!
Swala la madawa ya kulevya hata sina muda wa kuliongelea maana hao woooteee waliotajwa ni wauzaji madawa sio wa kwanza.. Walishatajwa weeengiiiiii na weeengiiii tuu, na bado wapo wana'survive na maisha yanasonga... Kila mtu aliye na maendeleo au maisha ya starehe basi muuza madawa..Hahahaaa... Ningepata ''evidence'' ningeweza find time to talk about it... Ila sijawahi kuona ''evidence'' hata moja zaidi ya maneno maneno tuu so siwezi poteza muda kuongelea ya kufikirika!!! AM OUT...
Nawapenda woteee,
I love Tanzania and I am Team Lowassa,
XOXO!!!
No comments:
Post a Comment