Let's talk about fashion. I love fashions and napenda kupendeza, na zaidi napenda pia kuwaona watu wamependeza...
Ngoja niwaambie siri yangu moja...mie sometimes napitiaga my wassap contacts naangalia profile pictures za watu na nikiona tuu mtu kaeka picha ambayo amependezaaaa, naiiba.. Hahahahaa, na mie nakuwa nimepata cha kuiga apo na hata nisipoweza kuiga mie basi nitamshauri mtu nae avae hivyo ili atoke bomba!!! Yeah,that's my secrete...
One thing I miss in fashion jamani ni high'hills...kiruuuu!!! Mie na viatu virefu siku hizi ni kama we devorsed to each other kabisaaaa... Zamani nilikuwa naviweza but after my first operation Doctor alinishauri nisivae viatu virefu hadi nipone (alisema sijui nitaumwa mgongo maana in operation nilichomwa ile sindano ya mgongoni) Then nikawa navaa tuu flats, for a year nikawa nimepona sasa badala ndio ningeanza kuvaa high hills zangu si nikabeba mimba yena, full mauvivu and 2nd operation sasa ndio naona kama kuvaa high hills ni adhabu.... Am not very proud about it!!!
So now nitaanza hata siku moja moja niwe navaa high hills hadi nirudie tena enzi zileeeee, na hivi now am 82kgs, hahahaaaa... God is soooooo good yaani, bado tuu 4kgs na mie niwe in 70's.... Nakazana, siku hizi napungua nusu kilo yaani and miezi mingine robo kilo duh!!! Wakati naanza diet I lost 4kgs faster, then 3kgs mmmh.... I wish niweze kupunguza more kgs jamani ila ni kama nime'stuck!!!!
Ooowky, back to fashion and fashionista's point... Kuwa fashionista sio mpaka awe na nguo nyingi kabati lako liwe kama Gf boutique, Noooo, kuwa fashionista ni kuwa m'bunifu wa nguo zako hizo hizo ulizonazo kila siku zikupe muonekano mpya!!
Fashionista unatakiwa uwe mtu wa kubadilika badilika, usiwafanye watu wakauzoea muonekano wako... Sio watu wakiona sketi ndefu tuu hata kwa nyuma wanajua ni wewe umepita, Noooo... Usikubali kusomeka yaani...
Alright, hapa ni baadhi ya ma'fashionista wanaojielewa wanavyoonyesha ubunifu wao wa nguo moja in different looks....
(Nguo ile ile ila ubunifu wako tuu utakufanya kila siku watu wakuone mpyaaaaaa) That's a real definition of being a fashionista!!!
Credits: Skittilish.
Amevaa same suti ila amepata muonekano tofauti mara nne..
Suti ni iyo iyo moja ila amebadilisha top, shirt, vest, shoes and pochi na akaonekana totally different kwa kila pose!!!
Credits: MusingsOfACurvyLady
Gauni moja tuu (white dress) ila kalifanya liwe na muonekano tofauti mara nne, kabadilisha viatu, pochi, belt, kaongezea denim kikoti kwa juu yaani anatokea tofauti tofauti with only one dress!!
Credits:Gf Collectionstz
Same blue leggings and white top ila imenipatia muonekano wa tofauti mara tatu kwa kubadilisha tuu viatu, style ya kufunga mikanda ya top, pochi, accessories na kuvaa kikoti kwa juu.
Credits: Soraya
Amevaa same blue dress ila amelipa muonekana wa tofauti mara tatu kwa kuongeza kikoti kwa juu, sweta kwa ndani, pochi na viatu vya tofauti.
Credits: Dida
Ni gauni fupi la geans ila juu kavalia top na kufanya kuonekana kama ni sket na top, and chini ni the same dress, different shoes, !!
Credits: Stella
Kavaa same geans na white top ila kajipatia muonekano wa tofauti kwa kuongezea koti refu, kikoti kifupi na pochi...
Duh!!! Kwa leo inatosha wapendwa... Hope na nyie mtapata mionekano tofauti kila siku, hata kama nguo ni zile zile waweza kuwa unabadilisha kitu kidogo tuu and you'll look totaly new each and eeeeeevry day!!!!
Kwa kupendeza zaidi karibu Gf-Boutique!!!
XOXO...
No comments:
Post a Comment